MMOJA wa mwili wa marehemu Elias Edward
(28)aliyekufa katika ajali ya gari la abiria (Haice) likihusisha basi la
Kampuni ya Allys iliyotokea Ijumaa iliyopita eneo la Buhongwa Jijini hapa
imegombewa na kuleta tafurani kubwa kwa familia nani achukue mwili huo kwa
ajili ya maziko.
Mvutano huo uliozua mabishano
makali kupelekea ugomvi wa kutupiana maneno yasiyofaa kati ya Mjane wa
marehemu Edward na upande wa baba wa marehemu aliyekufa katika ajali
uliohifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini hapa kufatia
mabishano hayo.
Habari zilizotufikia kuwepo na mvutano huo,
mazishi ya marehemu Edward yaliyokuwa yanatarajiwa kufanyika jana
mchana bado kilikuwa ni kitendawili baada ya kushindikana na hadi tukienda
mitamboni jana, kutokana na kutojulikana wapi na lini yatafanyika.
Kufatia ugomvi huo uliopo, umedaiwa kuwepo
baada ya mmiliki wa basi hilo la Kampuni ya Allys, kukubali kugharamia
mazishi ya marehemu huyo na wengine wa ajali hiyo yaliyotarajiwa kufanyika
jana Nyasaka Wilayani Ilemela alikokuwa marehemu amejenga na kuishi hadi
mauti yanamkuta ama Wilayani Misungwi alikozaliwa.
“Marehemu alikuwa akiishi na familia yake
na mke aliyetajwa kwa jina la Veronika Makoye na watoto watatu akiwa na
marehemu Edward” imefahamika.
Baadhi ya ndugu na waombolezaji wakizungumza
gazeti hili jana wakati wa sakata hilo katika Hospitali ya Bugando, mjane
na mama mzazi wa marehemu, Kulwa Daudi, walisema kuwa wao walitaka
marehemu akazikiwe nyumbani kwake lakini shangazi zake na baba zao wadogo
walipinga na kutaka wakazike kwao.
“Mrehemu mme wangu kwa zaidi ya miaka saba
hadi mauti ya ajali mbaya hii yalipomkuta,inanisikitisha wakwe zangu (shangazi
zake marehemu na baba zake wagogo) wakatae nisimzike mme wangu ….”
Aliesema huku akitokwa na machozi mjane huyo.
Kwa upande wake Mama mzazi wa marehemu huyo
Bi Daud aliungana na mjane huyo kwa kutaka mwili huo ukazikwe Nyasaka lakini
shangazi zake Misungwi, Tatu Misungwi na baba yake mdogo aliyefahamika kwa
jina moja la Mabula, walikataa na kutoa maneno makali kwa mjane, wakidai
yeye na mama mzazi wa marehemu, hawana maamzi kuliko wao.
“Sijawahikuona mke wa marehemu na familia yake
kupangiwa na mwinga (yani mjane) au shemeji (mama mzazi) marehemu ni mtoto
wetu, vinginevyo hatutaki, leo hatutazika hadi mahakama itakapotoa
maamzi.” Alidai Mabula huku baba mdogo mwingine wa marehemu (jina
halikupatikana mara moja) akitishia kuzuia ndugu wengine wa upande wao,
wasikanyage Nyasaka.
Ajali ya basi la Allys lenye namba za
usajiri T.961 AGP aina ya Scania, liligongana na Hiace T. 656 AQW katika
eneo la Buhongwa na kusabisha vifo vya watu tisa,saba kati yao akiwemo Edward
walikufa papo hapo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.