"Sasa tunazianza mbio kwa wanawake" |
MBIO
za Makasia za Balimi Extra Lager mkoa wa Mwanza,
zimemalizika juzi (jumamosi) kwa wapiga makasia wa Wilaya za Misungwi na Sengerema kushika nafasi ya
kwanza na pili.
Fainali ya mashindano hayo ya 14 ilifanyika kwenye ufukwe wa Kirumba Mwaloni, Manispaa ya Ilemela ambapo mshindi wa kwanza wanaume nafasi ya kwanza ilinyakuliwa na wapiga makasia kutoka Buyagu Sengerema, mtumbwi wakioongozwa na nahodha Costantine Lusajo na kunjinyakulia shilingi 900,000 kutoka kwa wadhamini TBL .
Washindi wa kwanza katika picha ya pamoja na meza kuu.
Nafsi ya pili ilinyakuliwa na mtumbwi wa Daniel Mgema wa Misungwi na kuzawadiwa sh.700,000,Leonard Sumbu alikabidhiwa kitita cha sh.500,00 na kuwafuta machozi wenyeji, wilaya ya Ilemela baada ya kushika nafasi ya tatu nakutinga fainali za mwaka huu zitakazo fanyika Desemba 7,mwaka huu.
Nafasi ya nne ilikwenda kwa mtumbwi wa nahodha Fabian na kupata sh 400,000, ambapo washiriki walioshika nafasi ya sita hadi ya kumi, walipata kifutajasho cha sh.250,000 kila mmoja kutoka kwa wadhamini. Wilaya ya Misungwi ilionyesha kupania mashindano ya mwaka huu baada ya washiriki wake kwa upandewa wanawake kuitwaa nafasi ya kwanza na kujinyakulia kitita cha sh.700,000 na kuzimangebe za Ilemela mwaka huu.Washindi waliongozwa na nahodha Taabu Daud.
Hawa ndiyo washindi wa kwanza wanawake mbio za makasia wakitokea wilaya ya Misungwi katika picha ya pamoja na meza kuu.
Nafasi ya pili ilinyakuliwa pia na wapiga makasia wa Misungwi wakiongozwa na nahodha Regina Kazungu, na kuzawadiwa sh.600,000. huku mtumbwi wa Happy Mnare wa Ilemela ukishika nafasi ya tatu na kuambulia sh.400,000 na nafasi ya nne ikitwaliwa na mtumbwi wa nahodha Advera na kupata sh.300,000. |
Washiriki wa michuano hiyo ya mitumbwi walioshika nafasi ya sita hadi ya kumi wao walipata kifutajasho cha sh.200,000 ambapo wilaya ya misungwi ambayo ilishikisha timu nyingi ikioneka kupata mafanikio.
Washindi wa tatu wajuu kwa wanaume na wanawake walioshika na nafasi ya kwanza na pili watatu wakilisha mkoa wa Mwanza kwenye fainali .
Alisema ni kwa kufanya hivyo, washindani wanaweza kushiriki michuano ya Olimpiki kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama hicho, Richard Mgabho,kwani ndiyo dhamira na malengo yao.
“Rai yangu kwa chama cha Makasia, mtuletee mashindano ya kitaifa, sababu uwezo tunao wakuyaendesha. Hatuwezi kwenda kwenye Olimpiki bila kuwa namashindano ya Kitaifa, lakini pia mwakani washiriki waje na vifaa kamamakasia badala ya kutegemea wadhamini pekee,” alisema
Aidha Mgabho alisema ada ya kushiriki wamashindano hayo kwa wasio wanachama itakuwa
sh.50,000 kwa wanaume nawanawke watalipa sh.30,000 na wanachama watalipa ada ya
sh.10,000.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.