Wadau wakiwa makini kusanyikoni. |
Kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia litapokelewa Mkoani Mwanza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa CCM Kirumba.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, mbele ya
waandishi wa habari na kamati ya maandalizi ya ujio huo katika ukumbi wa
Mwanza Hotel hii leo.
Ndikilo amesema kuwa hii
itakuwa ni mara ya kwanza kwa kombe hilo kugusa ardhi ya mkoa wa Mwanza hivyo amewataka
wanachi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kunakshi na kutia mashamsham ya ujio wa
kombe hilo lenye historia.
Naye Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambaye yupo ziarani katika Mkoa wa
Simiyu amekubali kuwa mgeni rasmi kulilaki kombe hilo litakalotua nchini katika
ardhi ya mkoa wa Mwanza kisha jijini Dar es salaam.,
Amesema kombe hilo
litawasili katika uwanja wa ndege wa mwanza majira ya saa tatu asubuhi na badae
kupelekwa katika uwanja wa CCM Kirumba, ambapo pamoja na mambo mengine baadhi
ya wananchi watapata fursa ya kupiga picha na kombe hilo.
Kwa upande wake Mwakilishi
wa Coca Cola Nchini bw. Eyebolt Gretchen, amesema ujio wa Kombe hilo kwa mara
ya tatu katika nchi ya Tanzania umekuja kutokana na utulivu na amani
iliyotawala nchini sanjari na ukarimu wa watu wake, Miongoni mwa nchi za Afrika
ambazo zimekuwa na utulivu hata kufanya kutembelewa na kombe la Dunia ni
Tanzania, amesema na kuongeza kwamba, kama Coca cola wamekuwa mstari wa mbele
kwenye jitihada za kukuza soka nchini ikiwapo mashindano ya Kopa Coca cola.
Kwa upande wake kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ernest Mangu amewahakikishia wanachi wote wa Mkoa wa
Mwanza amani na utulivu, aidha amewaomba wananchi kutokuja uwanjani wakiwa na
watoto wadogo ili kuepusha adha wanayoweza kupata watoto hao kutokana na
msongamano.
Hii ni mara ya tatu kombe
hilo kutua nchini ambapo mara zote
limekuwa likipokelewa na kulakiwa na wananchi waishio katika Mkoa wa Dar es
Salaam.
Ujio wa kombe hilo si tu
kwamba linakuja kutazamwa na wananchi wa Mwanza bali pia ni fursa nzuri kwa
mkoa huo kujitangaza kimataifa, kutangaza rasilimali zinazo patikana katika
Mkoa huo na lakini pia ni chachu kwa vingozi kuona kuwa kuna umuhimu wa kuipa
kipaumbele michezo yote.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.