Awali
akifungua mkutano huo uliokuwa ukijadili ajenda mbalimbali za uboreshaji sekta
ya afya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib
Bilal amesema serikali itajitahidi kuboresha mikopo kwa wanafunzi wanao soma
fani hiyo hivyo hawapaswi kujihusisha na migomo isiyokuwa na lazima.
Ameongeza
kuwa kwa sasa serikali imeongeza juhudi zake za kuboresha mazingira na vifaa
kwa hospitali nchini ili kuwafanya
madaktari wake na wataalamu wake kubakia nchini tofauti na miaka mingine ambapo
wengi wamekuwa wakikimbilia nchi za mbali kufanya kazi. Sikiliza mazungumzo kwa kubofya play....
Baada ya
wanafunzi Madaktari wa vyuo vya elimu ya juu nchini kutoa tamko la
kutoridhishwa na kiwango cha mkopo cha shilingi milioni 2,600,000/= wanachopata
kutoka bodi ya mikopo Tanzania kuwa hakikidhi mahitaji ya ulipaji wa ada,
hatimaye Serikali imekuja juu na kukanusha madai hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza baada ya ufunguzi wa Mkutano wa sita wa Kimataifa wa chama cha Madaktari Wanafunzi (TAMSA), Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Husein Mwinyi amesema kuwa Serikali inatoa mikopo stahiki kwa wanafunzi hao licha ya madai wanayosema.
Bofya play kusikiliza..
Inspirational Talk Mr. Richard Kasesela |
Meza kuu. |
Kusanyiko la Wanafunzi Madaktari kwenye mkutano wa sita wa kimataifa uliofanyika JB Belmont Mwanza. |
Eng. Evarist ndikilo The Region Commissioner of Mwanza. |
TAMSA |
Another angle. |
Human Resources for Health Crisis by Prof William Mahalu. |
Team. |
Mapinduzi ya Teknolojia na mwasilishaji mada ni Dr.Garvin Kweka. |
Wadau kusanyikoni. |
Speech from the Guest of Honour, Dr. Mohamed Gharib Bilal. |
Zawadi utoka TAMSA kwa mgeni rasmi. |
Zawadi toka kwa TAMSA kwenda kwa Waziri wa Afya. |
Picha ya Pamoja. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.