ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 1, 2013

NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE. STEPHEN MASELE NA RAFIKI ZAKE WACHANGIA MILIONI 50 UJENZI WA KANISA RC NYASAKA

Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele akiwatambulisha rafiki zake aliokuwa ameambatana nao katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Roman Catholic Kigango cha Mtakatifu Anthonio wa Pandua Nyasaka ambapo mheshimiwa na marafiki zake walitoa kiasi cha shilingi milioni 50 kuchangia ujenzi huo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele akitoa tamko wakati akiwatambulisha rafiki zake aliokuwa ameambatana nao katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Roman Catholic Kigango cha Mtakatifu Anthonio wa Pandua Nyasaka ambapo mheshimiwa na marafiki zake walitoa kiasi cha shilingi milioni 50 kuchangia ujenzi huo

Diwani wa Kata ya Mlangarini wilaya ya Arusha Mjini Mhe. Mathius Manga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Gold Crest Hotel Mwanza, akiwasilisha mchango wake kiasi cha shilingi milioni 3 kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Roman Catholic Kigango cha Mtakatifu Anthonio wa Pandua Nyasaka ambapo mheshimiwa na marafiki zake walitoa kiasi cha shilingi milioni 50 kuchangia ujenzi huo.

 Wajasiliamali  Sekta ya wachimbaji wadogo wadogo mkoani Geita wakiwasilisha mchango wao kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Roman Catholic Kigango cha Mtakatifu Anthonio wa Pandua Nyasaka ambapo mheshimiwa na marafiki zake walitoa kiasi cha shilingi milioni 50 kuchangia ujenzi huo.

Michango ikiendelea kumiminika.

Nao waratibu wakiendelea kutunza kumbukumbu.

Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele akihamasisha waumini kuchangia kwa nguvu zote kwenye harambee ya ujenzi wa Kanisa la Roman Catholic Kigango cha Mtakatifu Anthonio wa Pandua Nyasaka ili watoto na jamii kwa ujumla wapate eneo la kukusanyika na kujifunza maadili mema yenye tija katika ujenzi wa taifa la amani.
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele akiwa na diwani wa kata hiyo ya Nyakato Mhe. Manyerere (CHADEMA) ambaye naye alishiriki vyema kuchagiza mafanikio ya Harambee hiyo ya ujenzi wa Kanisa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele akiwa na Mhe. Mbunge Maria Hewa (CCM) ambaye naye alishiriki vyema kuchagiza mafanikio ya Harambee hiyo ya ujenzi wa Kanisa.

Sasa hapa mama akashika usukani.....

Hii ndiyo Ramani ya ujenzi wa Kanisa la Roman Catholic Kigango cha Mtakatifu Anthonio wa Pandua Nyasaka, ambalo pindi litakapo kamilika litakuwa na uwezo wa kuchukuwa zaidi ya watu 1,500 tofauti na kanisa la awali lisilo na uwezo wa kuchukuwa hata idadi ndogo ya watu 200.

Mchoro wa ramani hiyo ya kanisa kutoka juu.

Muonekano wa picha ya Kanisa la Roman Catholic Kigango cha Mtakatifu Anthonio wa Pandua Nyasaka.

Marafiki wa Mhe. Masele akiwemo Mr. Edgar Mapande (wa tatu kutoka kulia) wakisikiliza kwa umakini kile kinachojiri.

Picha ya pamoja kabla ya Mhe. Naibu Waziri hajaondoka eneo la Harambee kuwahi ratiba nyingine za utumishi kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele akiwaaga waumini waliojitokeza kwenye harambee ya ujenzi wa Kanisa la Roman Catholic Kigango cha Mtakatifu Anthonio wa Pandua Nyasaka 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.