ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 2, 2013

TTCL YAJUMUIKA NA WATEJA WAKE MKOANI MWANZA KATIKA CHAKULA CHA JIONI.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akitoa hotuba katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na TTCL Mwanza.

Tukio hili ambalo limefanyika mwishoni mwa wiki limefanywa na Kampuni ya Mawasiliano ya TTCL mkoa wa Mwanza ili kupata nafasi ya kukutana na wateja na kupata maoni yao ya jinsi inavyoweza kuboresha huduma zake na kukidhi  mahitaji ya mawasiliano  ili kupanua wigo wa kufanya shughuli za biashara, uchumi, kijamii na maendeleo.

Wadau mbalimbali toka mashirika binafsi na ya kiserikali wakisikiliza kwa umakini yanayojiri ndani ya Hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa JB Belmont Mwanza.

Dira ya TTCL ni kuwa mtoa huduma bora ya Mawasiliano nchini Tanzania katika viwango vya kimataifa, walengwa wakiwa ni wateja na nguvu ikiwa ni wafanyakazi.

Hadi sasa TTCL inatoa huduma za simu za maongezi na Data kupitia simu za mezani, simu za mkononi yaani TTCL mobile, Huduma za Data kwa maana ya maandishi na picha yaabi TCCL kupitia Broadband pamoja na Internet. 

Meneja wa TTCL Mkoa wa Mwanza (aliyesimama) akibofya simu ya mezani ya TTCL kuwaunganisha mameneja wote wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kuzungumza kwa pamoja kwa njia ya simu na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliyeketi na baadhi ya viongozi mezani.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo (katikati) akizungumza na mameneja wa mikoa ya Kagera, Shinyanga, Simiyu pamoja na Meneja msaidizi mkoa wa Mara, kupitia simu ambapo kwa sasa TTCL wanatumia teknolojia ya kuunganisha simu zaidi ya moja kufanya mazungumzo ya pamoja kwa wakati mmoja.

Katika ushauri uliotolewa na baadhi ya wadau ndani ya hafla hiyo waliishauri TTCL kuboresha huduma zao kuanzia upatikanaji wa vocha, mauzo ya laini zao pamoja na upatikanaji wa huduma za TTCL kila kona ya soko la nchi ili kuwanufaisha wananchi wapate huduma zilizo bora zinazoendana na ushindani wa juu uliopo.

Ili kuboresha huduma za mawasiliano mfanyabiashara maarufu wa jijini Mwanza Mohamed Gupta alipata fursa ya kutoa ushauri kwa TTCL.

Mmoja kati ya maafisa wa TTCL akisalimiana na baadhi ya waandishi wa habari.

Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko TTCL Peter Ngota akimkabidhi zawadi ya simu ya Smart phone Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo kwaajili ya mawasiliano madhubuti.

Mkuu wa mkoa akiainisha zawadi yake haflani.

Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko TTCL Peter Ngota akimkabidhi zawadi ya simu ya Smart phone Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Alifa Hassan Ida kwaajili ya mawasiliano madhubuti.

Meza kuu na picha ya pamoja na Viongozi waalikwa.

Meza kuu na picha ya pamoja na wateja wa TTCL.

Meza kuu na picha ya pamoja na wafanyakazi wa TTCL kanda ya Ziwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.