Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo amewashangaa watu wanaopinga pendekezo la Serengeti kuwa jina la uwanja wa Ndege wa kimataifa wa jijini Mwanza.
Watu hao wanadai kuwa uwanja huo hauwezi kupewa jinia hilo kwa kuwa Serengeti ipo mkoani Mara na si Mwanza.
Katika majibu yake wishoni mwa wiki kwa maswali ya waandishi wa habari waliomuuliza maswali wakati alipokuwa akizungumzia maandalizi ya wiki ya utalii iliyoanza leo (24/09/2013) jijini Mwanza, Ndikilo alihoji kuwa mbona Hotaeli ya Kilimanjaro ipo Dar es salaam wakati mlima Kilimanjaro upo mkoani Kilimanjaro.
Pia alitoa mfano wa bia ya Serengeti ambayo pia huzalishwa na kiwanda cha Serengeti Breweries kilichopo Igoma jijini Mwanza na kuhudumia kanda ya Ziwa.
Sehemu ya wahudhuriaji ikiwa ni waandishi wa habari na wadau wautalii waliohudhuria mkutano huo kwenye Ukumbi wa Mikutano ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. |
Wandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo ulioandaliwa na kamati ya kukuza utalii mkoa wa Mwanza uliofanyika ukumbi wa mikutano ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza. |
Hata hivyo amewataka wananachi kuondokana na mawazo ya kuwa utalii ni kwaajili ya watu wenye ngozi nyeupe tuu bali hata wananchi wenyewe wanayofursa ya kutenbelea vivutio vyao vilivyopo nchini kama sehemu ya elimu na burudani.
Akitoa mfano Ndikilo alisema nchini China asilimia 90 ya wachina ndiyo wanaotembelea vivutio vya utalii nchini mwao hivyo basi watanzania hawana budi kuiga utamaduni huo.
Ametaka siku ya utalii watu waondokane na dhana ya wageni ndiyo wenye fursa ya kutalii pekee badala yake wajenge utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii nchini.
Wiki ya utalii Kitaifa inafanyika jijini Mwanza katika uwanja wa Michezo wa Nyamagana ambako maonyesho yanafanyika, yakiendelea hadi kilele chake tarehe 27 September 2013
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.