Arsenal, Liverpool kisheko
*Manchester United, Spurs walizwa
*Manchester United, Spurs walizwa
Ligi Kuu ya England imeendelea kujifungua, ambapo Manchester United walidunguliwa na Liverpool huku Tottenham Hotspur wakiraruliwa na Arsenal.
Manchester United walio chini ya kocha mpya David Moyes aliyechukua nafasi ya Alex Ferguson hawakuamini kuoga bao moja lililofungwa na Daniel Sturridgre, ambapo jitihada zao zote za kupata walau sare hazikufanikiwa.
Baada ya kwend mapumziko walitarajiwa kurudi wakiwa wamebadilika kutokana na kupata maelekezo ya kocha Moyes lakini pamoja na kubadilili wachezaji hawakuweza kwenda na kasi ya mchezo.
Katika mechi nyingine, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anayeshambuliwa kwa kutosajili nyota alichekelea kwa kupata ushindi dhidi ya mahasimu wao wa London kaskazini, Tottenham Hotspur.
Arsenal walifunga bao pekee la ushindi kupitia kwa mshambuliaji Olivier Giroud aliyeweka kimiani mpira baad ya kupata majalo ya Theo Wilcott katika dakika ya 23 na lilidumu hadi mwisho.
Spurs walihangaika kupata matokeo tofauti, lakini jitihada zao ziliishia kwa ama golikipa wa Arsenal kudaka au kwa mipira kuwa mwingi.
Spurs walicheza bila winga wao, Gareth Bale anayesemwa kukamilisha usajili wake kwa miamba wa Hispania, Real Madrid.
Kwa matokeo ya mechi hizo, Liverpool inashika usukani kwa kushika nafasi ya kwanza, kwa rekodi nzuri ya kushinda mechi zake zote tatu za mwanzo na kufikisha pointi tisa.
Wanafuatiwa na Chelsea, Manchester City, Arsenal, Stoke, Spurs, Manchester United, West Ham, Norwich na Southapton.
Wanafuatiwa na Chelsea, Manchester City, Arsenal, Stoke, Spurs, Manchester United, West Ham, Norwich na Southapton.
Wanaoshika nafasi ya mwisho sasa ni West Bromwich Albion wakisaidiwa na Sunderland na Hull juu yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.