|
Ni muonekano wa J. A Hotel majira ya jioni. |
|
Mgeni rasmi wa ufunguzi wa J. A Hotel, Justus Molai (wa pili toka kulia) ambaye alikuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Urambo mkoani Tabora, akikata utepe kuashiria uzinduzi huku akipewa tafu na Mkurugenzi wa hoteli hiyo Bw. Asenga (wa kwanza kulia) na wadau wengine wakishuhudia tukio hilo. |
|
Mara baada ya ufunguzi wageni waalikwa walipata fursa kuzuru mazingira ya ndani na nje ya Hoteli J.A iliyopo barabara ya Rufiji jijini Mwanza. |
|
Mapokezi. |
|
Korido. |
|
Vyumba na muonekano. |
|
Rooms. |
|
Wahudumu. |
|
Wahudumu. |
|
Jikoni. |
|
Sisters wakiwa wamebeba kinywaji cha asili aina ya mbege ambacho kilitumika kama sehemu ya shangwe za mafanikio ya hafla ya ufunguzi. |
|
Mgeni rasmi pamoja na mmiliki wa J. A Hotel wakifaidi ladha ya kinywaji cha ufunguzi. |
|
Chiazzz kwa wadau wote. |
|
Meza hadi meza kwa waalikwa. |
|
Tusherehekee.. |
|
Misosi time...... |
|
Mgeni rasmi wa ufunguzi wa J. A Hotel, Justus Molai ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Urambo mkoani Tabora akizungumza kwenye hafla hiyo |
MWANZA: Wafanyabiashara
jijini Mwanza wametakiwa kutumia fursa ya mkoa huu kuwa kitovu cha biashara kwa
nchi za Afrika Mashariki kwa kujenga kumbi kubwa za mikutano pamoja na hotel.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo wa hotel yenye hadhi ya nyota mbili ya J.A iliyopo jijini Mwanza Justus Molai
ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Urambo alidai kuwa Mwanza ni mji
ambao unakuwa kwa kasi kutoka na rasilimali ziliziopo hivyo ukuaji wake unatakiwa kwenda sambamba na huduma zinazopatikana.
“Huu ndo wakati wenu wa
kuchangamkia fursa hiyo tofauti na kuwa Mwanza kitovu cha biashara kwa nchi
hizo pia ni mkoa ambayo utakuwa na watalii wengi kutokana na vivutio vilivyopo
kama mbuga za wanayama,ziwa pamoja na mapango waliyokuwa wakiishi
wajerumani”alisema Malai.
Aliendelea kwa kusema
kuwa serikali kwa upande wake inaendele kutengeneza miundombinu ya
reli,barabara na viwanja vya ndege na kuwahimiza kutumia nafasi hiyo kuwa
wabunifu katika biashara ili kila mgeni atakaye ingia Mwanza asipate sababu ya
kwenda nchini hizi za jirani kutembea.
Alisema kuwa uwanja
ndege ukikamilika itakuwa rahisi wafanyabiashara kufika katika nchi hizo tatu
za afrika Mashariki ongozeko la wafanyabiashara kuingia mkoani hapa litakuwa
kubwa na uchumi wa mkoa utaongeza pamoja na nchi kwa ujumla kwasababu kutakuwa
na ongezeko la fedha za kigeni.
“Nampongeza Asenga kwa
kuona fursa hii ya kujenga hoteli ya kisasa kwa sababu ameiona fursa hiyo na
ameitumia lakini hii haitoshi mnatakiwa na nyie kufuata nyayo hizo katika
kuhakikisha kuwa mnabuni vitu vingine vya kufanya ili
muweze kujitanua katika biashara”alisema Molai.
Hata hivyo aliwataka
wafanyabiashara wakubwa nchini kuwasaidia wale wadogo ili waweze kuinuka hasa
katika kupata mitaji kwa kupitia taasisi za fedha ambapo kunaonekana
kunaurasimu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.