ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, September 29, 2013

DIAMOND AWAOMBA RADHI MASHABIKI FIESTA MWANZA KUPIGA SHOW LEO USIKU NA SKYLIGHT BEND

NA ALBERT G. SENGO MWANZA:

Msanii wa Kimataifa tokea nchini Tanzania Diamond Platnum ambaye alikuwa akisubiriwa kwa hamu kutumbuiza kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza amewaomba radhi mashabiki na waandaaji wa Tamasha hilo kwa kushindwa kufanya hivyo jana mara baada ya kukwama njiani akikosa kivuko akitokea Mkoani Geita ambapo pia usiku huo huo alikuwa akipiga show.

Diamond Platnum ambaye alikuwa akisubiriwa kwa hamu na kiu kubwa na mashabiki wake amesema kuwa tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya licha ya juhudi alizokuwa akizifanya usiku wa jana kuhakikisha anafika uwanja wa CCM kirumba na kukonga  nyoyo za mashabiki wake.

Hata hivyo msanii huyo usiku wa leo ataungana na Skylight Bendi kwenye Fiesta After Part itakayofanyika leo usiku Hotel Gold Crest... ZAIDI MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY.

Tupe maoni yako

1 comments:

Note: Only a member of this blog may post a comment.