Airtel yawanoa maafisa waTRA jinsi ya kulipia ada za lesseni za magari kwa Airtel Money
• Airtel yaendesha semina ya uelewa ofisi za TRA Mwenege -Dar es salaam
• Mafunzo ya kulipia kodi kwa Airtel Money wiki hii kuendelea Manzese,
Tegeta Myfair kisha mikoa yote nchini
Mwishoni mwa wiki hii Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea na ushirika wake na mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa kuanzisha semina za mafunzo kwaajili ya maofisa wa mamlaka hiyo ya jinsi ya
kurahisisha kukusanya mapato ya serikali kwa urahisi zaidi kupitia huduma ya Airtel Money
Mbinu pekee zinazoijadiliwa katika semina hiyo ni ile yakuhakikishamlipa kodi yeyote anapata fulsa ya kufahamu njia rahisi na zenye kuokoa muda pale anapotaka kufanya malipo ya kodi mambali mbali ikiwemo ya ada za lesseni za magari, ada za uamisho wa magari pamoja na malipo mengine ya ada za usajili wa magari
Mwishoni mwa wiki hii akiongea kuhusu ushirikiano huo wa Airtel Money na TRA kwenye ofisi za TRA MWENGE Afisa Mafunzo wa Airtel Bw, Elly Mgumba alisema “ tumeanza na wadau wetu wa TRA Mwenge-Dar es salaam lakini wiki ijayo tutasambaa mikoani ili wote wafahamu na waendelee
kuwaonyesha wananchi jinsi wanavyoweza kulipa ada zao
“Mteja akipiga *150*60# ataingia katika orodha yetu ya Airtel Money na kwenda moja kwa moja kwenye neno TRAMAGARI na kufanya malipo papo hapo” alisistiza Bw, Mgumba
Kwa upande wake Meneja Mradi wa Airtel Money John Ndungu alisema “Mafunzo haya ya kulipia kodi kwa Airtel Money wiki hii yataendelea katika mitaa na ofisi za TRA Manzese, Tegeta Myfair na kisha kuingia kutoa elimu haraka kwa mikoa yote nchini tukishirikiana na TRA idara ya elimu kwa mlipa kodi”
Lengo letu Airtel ni kuwafikia walipakodi ambao wanatamani kuokoa muda kwa kuepuka kukaa foleni kwenye ofisi za malipo na sasa walipie kwa huduma hii ya Airtel Money rahisi na salama na kisha kwenda kuchukua leseni zao kwenye ofisi yeyote ya TRA iliyopo karibu yako, alimaliza kusema Bw Ndunguru
Nae Afisa kodi wa TRA, Bw. Alex Dennis Mwenge aliipongeza Airtel kwa jitihada zake za kuipunguzia serikali usumbufu wa kukusanya kodi na kuwawezesha wananchi kulipa kodi kwa hiari ili serikali iweze
kuendelea na mambo mengine ya maendeleo ya nchi
“Ninawapongeza sana timu ya Airtel Money kwa kuja kututembelea na kujadili jinsi tunavyoweza kuokoa muda wa mteja wa Airtel kulipa kodi kwa urahisi kwa njia hii ya Airtel Money sasa kwa pamoja tutahakikisha wananchi wanaokuja kulipa kodi kwa hiari wanafahamishwa kuhusu Airtel Money ili waweze kulipa kodi zao BURE wakiwa mahali popote nchini”
Airtel Tanzania kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania TRA ilizindua rasmi huduma ya kufanya malipo ya ada za leseni za magari kupitia huduma ya Airtel money wiki mbili zilizopita. Huduma hii
inapatikana BURE yaani (Hakatwi Mtu Hapa) kwa wateja wote wa Airtel nchi nzima.
Huduma ya Airtel money pia inawawezesha wateja kutumia simu zao za mkononi kulipa bill ya maji DAWASCO, kulipia Luku TANESCO malipo ya DSTV, kulipia visa ya USA na sasa ada za lesseni ya magari. Airtel money ni huduma rahisi na salama inayopatikana kwa kupiga *150*60# na ufanye malipo mbalimbali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.