SAFARI BIKE RACE 2013 KUFANYIKA KESHO MKOANI
SHINYANGA
Mashindano ya mbio za Baiskeli kwa Kanda ya
Ziwa yajulikanayo kama “Safari Lager Bike Race 2013” yanatarajiwa
kufanyika kesho hapa Mkoani Shinyanga.
Shindano hilo ambalo limekuwa likifanyika
kila mwaka kwa kushilikisha mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Tabora,
Kigoma, Musoma, Kagera, Simiyu, Geita na Shinyanga limekuwa na mvuto wa kipekee
kwa wanywaji na washabiki wa bia ya Safari Lager kwani kushiriki kutoka katika
mikoa yote kwa kushindanisha mkoa upi kinara ya Kanda ya Ziwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani
Shinyanga mahali ambako mashindano yanafanyika, Meneja mauzo wa TBL Shinyanga,
Robert Kazinza amesema kuwa lengo hasa la Bia ya Safari Lagera kudhamini
mashindano haya ni kufufua mitaji ya wajasiliamali kanda ya ziwa kwani michezo
ni ajira na zawadi za mashindano hayo ni kubwa.
Mbio zitakazohusishwa ni
pamoja na mbio za wanaume ambao watakimbia Km 210, mbio za kimama Km
130, Mbio za walemavu wanaume na mbio za walemavu wanawake.
Pamoja na hayo chachu kuu
ya mashindano hayo inatajwa kuwa itakuwa ni zile mbio za kiubunifu toka kwa
akinamama watakao timua mbio na ndoo kichwani..
CHEKSHIA VIDEO INAYOFUATA HAPA CHINI:-
CHEKSHIA VIDEO INAYOFUATA HAPA CHINI:-
MWISHO.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.