Jiji hilo ambalo zamani lilisifika kwa kuwa na viwanda vingi hivi sasa limechakaa ambapo hata taa zake za barabarani hazifanyi kazi.
Detroit kwa sasa ni jiji bovu ambalo maandari yake yamejaa magofu ya nyumba zilizokuwa za makazi na maghorofa marefu yaliyotelekezwa pamoja na viwanda vilivyochakaa.
Pia vitendo vya uhalifu vimekithiri katika jiji la Detroit itaathiri pia manispaa na miji mingine ya jimbo la Michigan na majimbo mengine ya Marekani kuhusiana na kuaminika kwake katika kupata mikopo ya benki kwaajili ya maendeleo yake.
Gavana wa jimbo la Michigan Rick Snyder amesema ilikuwa lazima jiji hilo lifilisike kutokana na hali ya mambo ilivyokuwa ikienda katika uendeshaji wake.
Kutokana na jiji la detroit kukumbwa na hali mbaya, idadi ya wakazi wake pia imekuwa ikipungua mwaka hadi mwaka kutokana kuwa na wakazi milioni 1.8 mwaka 1950 hadi kuwa na wakazi 700,000 tu hivi sasa.
Misukosuko ya ubaguzi wa rangi iliyosababishwa na wanaharakati wa haki za binadamu pamoja na machafuko makubwa yaliyotokea mwaka 1967 mjini Detroit ni miongoni mwa matukio yaliyosababisha wazungu na watu wengine wa kipato cha kati kulikimbia jiji hilo, hali iliyodumaza shughuli za kibiashara na hivyo kushusha makusanyo ya mapato jijini humo.
Nyumba nyingi hazina watu kabisa zimegeuka kuwa magofu.
Detroit ndilo jiji lenye watu wengi zaidi katika jimbo la Michigan nchini Marekani lilikuwa makao makuu ya kaunti ya wayne ambayo ndiyo kaunti yenye watu wengi zaidi jimboni Michigan.
Jiji la Detroit ambalo lilianzishwa julai 24,1701, ikiwa ni kabla ya uhuru wa Marekani lina bandari kubwa iliyopo kwenye mto Detroit unaomwaga maji yake kwenye maziwa makuu ya Marekani hadi katika mkondo wa bahari wa St. Lawrence.
Likiwa limeanzishwa na mfanyabiashara mmoja wa Kifaransa jiji la Detroit lilisifika kwa kutengeneza magari ya Cadillac ambayo ni ya kifahari nchini humo na kwingineko duniani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.