ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 10, 2013

SALVATION YATWAA UBINGWA UMOJA CUP MARA BAADA YA KUILAZA 2-0 KISIMA CHA BURUDANI

Timu ya Salvation Fc ikikabidhiwa Ng'ombe mara baada ya kuibuka washindi wa Kombe la Fainali za Umoja Cup 2013, mara baada ya kuifunga timu ya Kisima cha burudani bao 2-0 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Goli la pili linafungwa kipindi cha pili katika dakika ya 88 mfungaji akiwa ni Emmanuel Mathew (anayepongezwa jezi namba 8 kwenye bukta)

Kabla ya goli hilo la pili Kisima cha Burudani katika dakika ya 75 ya kipindi cha pili walipata nafasi ya kusawazisha mara baada ya mmoja kati ya mabeki wa Salvation Fc kuunawa mpira kwenye eneo la hatari lakini kwa mshangao wa wengi mpigaji alikosa penati penati hiyo

Umoja Cup ni Mashindano yanayoandaliwa na Umoja wa Vijana CCM kata ya Nyamanoro yameamsha msisimko wa soka kwa vijana hali iliyosababisha mashabiki wa soka waliobahatika kuhudhuria fainali hiyo kuwa na kiu ya mashindano kama hayo tena na tena. 

Patashika za hapa na pale...

Ni mara baada ya mwamuzi wa mchezo huo kupuliza kipyenga cha mwisho kuashiria mpira finito.

Mashabiki vijana na mwamko wao.

Shangwe za vijana wa Salvation mara baada ya kuibanjua 2-0 Timu ya Kisima cha Burudani.....

Doto Joseph ambaye ni kocha mchezaji wa timu ya Kisima cha Burudani akipokea zawadi za mshindi wa pili wa Umoja Cup ambazo ni Jezi seti moja, mpira na kisha baadaye alikabidhiwa mbuzi mnyama.

Kapteni wa timu mabingwa wa Umoja Cup Salvation Fc akipokea zawadi ya jezi seti moja, mpira, kombe na walikabidhiwa ng'ombe mnyama. 


Kombe kwa mabingwa Salvation Fc.

Timu iliyokamata nafasi ya Tatu ni Afa Academy ambapo kwa upande wao waliondoka na zawadi ya mbuzi mnyama.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.