Jeneza lililoubeba mwili wa marehemu Humphrey Simon likiwa limewasili Nyumbani kwake Nyakato Sokoni kwaajili ya heshima za mwisho na kukesha kisha kesho asubuhi safari kuelekea Musoma kwa mazishi. |
Wakati ukipokelewa nyumbani kwake toka hospitali ya rufaa Bugando. |
Mc Bonke akiongoza shughuli na taratibu nzima msibani. |
Mjomba wa marehemu Archtc. Tega akitoa taratibu za jinsi familia ilivyopanga juu ya safari ya mwisho ya kuuhifadhi mwili wa marehemu. |
Ilikuwa ni majonzi wakati mke wa marehemu Humphrey Simon, Bi Neema akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu mumewe ambaye walifunga ndoa mwaka juzi tu (2011) |
Ndugu jamaa na marafiki wakitoa heshima zao za mwisho. |
Hatua za kuuaga mwili wa marehemu zikiendelea kwa upande wa akinamama. |
Bibi wa marehemu alipata wakati mgumu. |
Marafiki wa marehemu wakiuaga mwili wa marehemu mbele ni Mr.Dinno akifuatiwa na Mr. Chacha. |
Mjomba wa marehemu akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu mwanaye. |
Huzuni kwa marafiki: Dada Less akiuaga mwili wa marehemu. |
Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu ilifanyika jioni ya leo kisha mwili utalala hapa nyumbani kwa marehemu ambapo kesho jumamosi asubuhi safari kuelekea Musoma itafanyika kwajili ya mazishi. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.