ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 12, 2013

MKAPA AFANYA ZIARA FUPI YA GHAFLA KUIMARISHA UTENDAJI OFISI ZA CCM MKOA MWANZA

Rais Mtaafu Mhe. Benjamin William Mkapa akisaini kitabu cha wageni ofisi za CCM mkoa wa Mwanza ambapo alifanya ziara ya kuimarisha Chama kiutendaji kwa kazi za ndani.

Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya masuala muhimu ya chama mbele ya Rais Mstaafu pamoja na makada na viongozi wa ngazi mbalimbali mkoa wa Mwanza.

Wafanyakazi wa CCM mkoa wa Mwanza walijumuika na kikao hiki cha ghafla kilichofanywa na Mhe. Rais mstaafu.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Mwanza akitoa malezo ya hatua na maendeleo ya umoja wake mbele ya Mhe. Rais mstaafu Ben Mkapa.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akitoa malezo ya jinsi kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza ilivyojipanga kuhakikisha wananchi wanaishi salama bila hofu .

Mhe. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akitoa maelekezo na uzoefu kwa makada na viongozi wa CCM mkoa wa Mwanza hii ilikuwa mapema leo kabla ya kushiriki hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la BMC inayofanyika leo usiku Gold Crest Hotel Mwanza.

Mkapa akiagana na wadau wa CCM mkoa wa Mwanza mara baada ya kumaliza kikao hicho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.