MBUNGE wa Jimbo la Rorya Mkoani Mara Lameck Airo (La-Kairo) amesikitishwa na kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje kumtapeli kiasi cha fedha shilingi milioni moja alizozitoa ili zikatangazwe kama sehemu ya mchango kwa lengo la kuchangia harambee aliyoiendesha katika kijiji cha Buchile Kata ya Mkoma Mjini Shirati Mkoani Mara alikozaliwa Wenje.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya tukio la hivi karibu la Bw. Wenje kutumia jukwaa la harambee hiyo ya kuchangia elimu katika kijiji cha Buchile kumkashifu kwa maneno yasiyofaa Mbunge wa jimbo la Rorya na kusema kuwa mbunge huyo hajafanya maendeleo yoyote kwa watu wa jimbo lake licha ya kusaidiwa kuongea Bungeni.
Bw. Airo alisema kwamba kitendo alichokifanya Bw. Wenje cha kushindwa kuwasilisha mchango wa shilingi milioni moja alioutoa Airo katika harambee hiyo, kumchafua kwa kutumia lugha chafu pamoja na kushindwa kutambua thamani ya kazi mbalimbali ambazo amekuwa akizifanya katika kijiji hicho alikozaliwa Mbunge Wenje ni kitendo kisicho na uungwana na hakipaswi kufanywa na mtu wa hadhi yake anayetizamwa kama mfano wa kuigwa na jamii.
"Nadhani Bw.Wenje anapaswa kushindana nami kwa kwa vitendo katika kuwaletea maendeleo wananchi wa majimbo yetu badala ya kuhangaika na maneno jukwaani bila vitendo, hili haliwasaidii wananchi ila ninaamini mwisho wa siku tutakapokwenda kwenye tathimini tutaona ni nani aliwatumikia wananchi wake waliomchagua kikamilifu" "Mimi sitafuti umaarufu kwa wananchi wa Rorya na wao wanatambua hilo bali ni mimi niko kwaajili ya kutekeleza nilichowaahidi" alisisitiza Bw.Airo.
Mbunge Ezekiel Wenje. |
“Nimeshangazwa kuona hata michango yetu mimi shilingi milioni moja na Mwenyekiti wangu wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Bw.Charles Ochele aliyetoa laki tano hazikutajwa zaidi ya Bw. Wenje kutoa milioni moja tu kwenye harambee hiyo fedha aliyodai imetoka mfukoni mwake, hii inaonyesha kuwa hakuwa na harambee ya kweli bali lengo lilikuwa kuwachafua na kuwakashifu kwa maneno yasiyofaa viongozi wenzake ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa” alisema Airo.
Bw. Airo amesisitiza kwamba kamwe hatomjibu kwa matusi mbunge Wenje na badala yake atamjibu kwa vitendo kwenye utekelezaji shughuli za maendeleo kupitia ilani ya CCM.
Jimboni Rolya ahadi nyingi zilizoainishwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010-2015 hadi sasa miradi mingi inatajwa kukamilika kwa asilimia 90 huku mbunge wa jimbo hilo akiahidi kukamilisha miradi mingine iliyoainishwa mapema zaidi hata kabla ya kumalizika kwa msimu.
Hii ni mara ya pili sasa kwa Bw.Wenje kushutumiwa na Bw.Airo kwa kutoweka wazi michango ya fedha anazoomba kuchangiwa kwenye harambee mbalimbali alizoendesha akidai kusaidia maendeleo lakini imekuwa tofauti kwani michango kuwasilishwa pungufu ya idadi iliyotolewa na zaidi Wenje amekuwa akimshambulia kutumia mikutano ya hadhara na majukwaa ya kisiasa akidai kuwa hajatoa mchango wowote japo amemuomba kufanya hivyo.
BOFYA HAPA kusoma sakata lililopita http://gsengo.blogspot.com/2012/12/mbunge-wa-jimbo-la-rorya-bw.html
BOFYA HAPA kusoma sakata lililopita http://gsengo.blogspot.com/2012/12/mbunge-wa-jimbo-la-rorya-bw.html
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.