ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 21, 2013

MEYA WA KAMPALA APIGWA NA POLISI

Meya wa mji mkuu wa Uganda, Kampala anasema amepigwa na polisi waliofyatua risasi za mipira kuutawanya umati wa wafuasi wake.
Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa Lukwago huku wakimjeruhi
Akizungumza na BBC akiwa kitandani hospitalini, meya huyo Erias Lukwago, anasema alizirai baada ya gesi ya kutoa machozi ilipotupwa ndani ya gari lake.

Anaeleza kwamba maafisa wa polisi walimpiga kifuani na kuzirarua nguo zake wakimshutumu kwa kuchochea ghasia.
Meya huyo ni mpinzani wa rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.
Mtu mmoja anaripotiwa kufariki na wengine kadhaa kukamatwa wakati wa ghasia hizo.
Hata hivyo polisi wamekanusha madai ya kumpiga meya huyo , ambaye pia ni mkoasji mkubwa wa rais Museveni.
Upinzani unasema kuwa serikali inajaribu kukandamiza kilio cha mageuzi nchini humo.
Katika tukio lengine, kiongozi wa upinzani Kizza Besigye alikamatwa kwa kuandaa mkutano ambao polisi hawakuuidhinisha.
Bwana Lukwago, jana alikuwa anaelekea kwenye jopo maalum kwa mara ya kwanza ambayo huenda ikamwondolea wadhifa wake kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi.
Mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga mjini Kampala anasema kuwa polisi walizingira nyumba yake na kisha kumpeleka ambako jopo lilikuwa linaendesha vikao vyake.
Lakini akiwa anapelekwa polisi walirusha vikebe vya gesi ya kutoa machozi, ndani ya gari lake.
Alisema kuwa polisi walimgonga kifuani na kumrarulia nguo zake.
"walinipiga kifuani na kudai kuwa nachochea ghasia , walinirarulia nguzo zangu na kunitesa kwa kila njia. Nilijaribu kuwaambia waniache lakini sikufanikiwa,'' alisema Lukwago.
Kizza Besigye amedaiwa na polisi kuchochea umati wa watu mjini Kampala ili kumuunga mkono bwana Lukwago, kosa ambalo ofisi yake imanusha .
CHANZO/bbc swahili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.