ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 8, 2013

INTERNATIONAL INSPIRATION YAPANIA KUIMARISHA NA KUBORESHA MFUMO WA MICHEZO NCHINI

Afisa Michezo Mkuu wa Chuo cha Michezo Malya Alen Alex akizungumza na wadau wa michezo mkoa wa Mwanza katika warsha ya siku moja ya harakati za kuunda mfumo wa michezo nchini ambapo warsha hiyo iliwahusisha waalimu wa michezo kutoka shule za sekondari na vyuo, maafisa michezo wa Halmashauri, viongozi wa vyama vya michezo mkoa wa Mwanza.

Warsha hiyo imefanyika mkoani Mwanza chini ya usimamizi wa Internation Inspiration iliyo na kazi kubwa mbili kuangalia mfumo wa elimu kwa michezo na hisibati yake. 
Wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa elimu ya michezo nchini kwa minajili ya kuvumba vipaji na kuimarisha ushiriki wa michuano mbalimbali lakini kila mkufunzi amekuwa akifanya vile anavyoona yeye kwake inamfaa kulinganana malengo yake.

Sasa Wizara ya Habari na Michezo kupitia Mradi wa Internation Inspiration wamenuia kutengeneza mfumo ambao utatumiwa na waalimu wote ili kutengeneza daraja linaloaminika lenye vipaji vya kueleweka vilivyopitia misisngi tambuka ya michezo.
Wadau wa michezo katika warsha hiyo.
Makocha wanaofundisha vilabu ngazi za juu mathalani Premium league hawatojikita kwa sana kufundisha misingi ya soka suala ambalo ni la ngazi za awali kabisa, Mathalani:- kumiliki mpira, kutafuta pozisheni na kadhalika bali watajikita kufundisha mbinu za ziada za kiufundi kuishinda timu pinzani mara baada ya kuisoma kupitia mfumo wanao tumia na kadhalika. 
Wanawarsha kusanyikoni.
Tumeshuhudia makocha wengi hapa nchini hususani wageni wamekuwa wakitaabika sana kufikia malengo waliyowekewa na waajili wao kutokana na kushindwa kumudu wachezaji wetu ambao wengi wanavipaji binafsi na si misingi ya soka kama inavyotakikana.

Makocha hao wamejikuta wana programu ndefu ya ufundishaji kufundisha mbinu mpya za ngazi ya juu pamoja na kujumuisha pia yale yaliyopaswa kufundishwa kwa wachezaji hao kama ufunguo au msingi wa kuujua mchezo. 
Wadau wakichanganua mapendekezo kufikiwa uundwaji wa Mfumo wa michezo nchini.
Kazi iliyofanyika kwenye warsha hii ya wakufunzi na wadau wa michezo mkoani Mwanza ni kupokea maoni ya wadau hawa ambapo walipewa makabrasha ya miongozo ya mifumo na kuyapitia kubaini mapungufu na kutoa mapendekezo kulingana na hali na mazingira ya nchi. 
Afisa Michezo Mkuu wa Chuo cha Michezo Malya Alen Alex akizungumza na wadau wa michezo mkoa wa Mwanza katika warsha ya siku moja ya harakati za kuunda mfumo wa michezo nchini ambapo warsha hiyo iliwahusisha waalimu wa michezo kutoka shule za sekondari na vyuo, maafisa michezo wa Halmashauri, viongozi wa vyama vya michezo mkoa wa Mwanza.

Picha ya pamoja.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.