Mahakama makuu ya mjini Mogadishu Somalia yamemwaachilia huru mwandishi wa habari ambaye alifungwa kwa sababu ya kumhoji mwanamke aliyesema amebakwa.
Katika kesi iliyolalamikiwa kimataifa, mwandishi huyo, Abdilaziz Abdinuur, awali alipewa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja kwa kumhoji mwanamke ambaye alisema alibakwa na wanajeshi wa serikali.
Mwanamke huyo piya alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja lakini kesi yake ilifutwa kwenye rufaa awali mwezi huu.
Jaji wa mahakama makuu - Aidid Abdulahi Ilkahanaf - alisema mashtaka yote dhidi ya mwandishi huyo wa habari sasa yamefutwa.
CHANZO: bbc swahili
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.