Mwanamuziki wa muziki wa injili ambaye pia ni produza toka K Records ya jijini Mwanza, Goodluck Gozbert (pichani) tayari amethibitisha kushiriki katika kusanyiko la Pasaka Gospel Festival litakalofanyika ndani ya uwanja wa CCM Kirumba tarehe 31/03/2013 ambapo humo ndani atakutana na wakali wengine kama Enock Jonas anayetamba na wimbo 'Zunguka' , Neema Mwaipopo 'Raha jipe mwenyewe' na wengine wengi waliothibitisha .
Sikiliza songi lake jipya hapa chini.
BIOGRAPHYGoodluk Gozbert ukipenda waweza tumia jina lake la jukwaani Gozbert, ni msanii wa muziki wa injili nchini Tanzania toka Rock City (Mwanza).
Alizaliwa mnamo mwaka 1991 na kuanza kuonyesha kipaji chake mapema tu mwaka 2005 akitumikia kwaya ya Tumaini ya kanisa la KKKT Imani Mwanza.
Haikumchukuwa muda kwenda solo kwani mnamo mwaka 2008 akiwa na miaka 16 vilevile bado yu mwanakwaya wa Tumaini alifanikiwa kuachilia single zake za awali na hatimaye album iliyokwenda kwa jina NIMELIPIWA DENI, akimshirikisha Michael Malagila, akiirekodi ndani ya studio za Ujumbe Records Mwanza, chini ya maproduza Selemani Muyomba na Charles Sokoro.
Akikulia kwenye viunga vya kitongoji cha Ghana Kirumba jijini Mwanza Goodluck ni mtoto pekee wa Bw. Gozbert Rweyemamu na Bi. Janeth Gozbert, baba yake alifariki dunia mwaka 1992 wakati Goodluck akiwa mdogo (umri wa mwaka mmoja tu) hivyo mama yake alimlea kwa msaada wa Good Summaritans pamoja na marafiki wa mama yake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.