ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 19, 2013

WANAFUNZI SAUT WABISHA HODI OFISI ZA MKUU WA MKOA KUOMBA NAULI KWENDA BODI YA MIKOPO KUJUA HATMA YAO

Zaidi ya wanafunzi 300 wa Chuo cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) Campas kuu ya Nyegezi jijini Mwanza jana majira ya alasili waliandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakitaka wapatiwe nauli ya usafiri wa kwenda Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu jijini Dae es salaam kwaajili ya kushughulikia madai ya fedha zao kutokana na kukabiliwa na hali ngumu ya maisha chuoni hapo.
Sikiliza kisa na sababu za wanafunzi hawa wanaoishi sasa katika kipindi kigumu kiasi cha kuweka mali zao rehani kupunguza makali ya maisha na hatimaye kubisha hodi ofisi za mkuu wa mkoa kuomba msaada.

Mwanafunzi huyu anasimulia kuwa Baadhi ya wanafunzi wenzake chuoni hapo wamediriki kutumia miili yao kujiuza ili kupunguza makali ya maisha kiasi cha kupelekea baadhi ya wasichana kuunda urafiki wa mapenzi na wachuuzi wa vyakula ili wapate sahani ya chips, siku ipite. Bofya play Msikilize 
Ni hali ngumu, wasijue wapi ulipo kmwanga, hatimaye ombi lao ni kufika bodi ya mikopo kujuwa hatma yao. Sikiliza zaidi hapa..
Makundi na makundi  ya wanafunzi yalizidi kumiminika ofisini hapa lakini hadi tunakwenda mitamboni hatukuweza kufanikiwa kujua hatma yao, hata hivyo blogu hii italifuatilia suala hili kwa ukaribu kujua kinaga ubaga.
.

Wasijue la kufanya.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.