CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa muda wa siku 14 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na Naibu wake, Philip Mulugo kuhakikisha wamejiuzulu nyadhifa zao.
Kauli hiyo ya Chadema imetolewa na mwenyekiti wake taifa, Freeman Mbowe wakati alipokuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara, uliofanyika leo katika viwanja vya Furahisha Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ikiwa ni ufunguzi wa Baraza la viongozi wa Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi.
Mbowe ambaye aliongoza maandamano makubwa ya magari na pikipiki kuelekea uwanjani hapo, alisema, Waziri Kawambwa, Naibu wake, Mulugo pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, wameshindwa kuiongoza sekta hiyo muhimu, ndiyo maana kwa sasa wanafunzi wanaishia kuandika matusi na kupata alama 0 katika mitihani ya kuingia kidato cha kwanza.
Alisema, Waziri huyo ni lazima ajiuzulu nafasi yake hiyo, kwani taifa ameliingiza pabaya na kuanza kuzalisha maelfu ya watoto wa masikini kumaliza elimu zao za msingi na sekondari hawajui kusoma na kuandika, na kwamba Waziri Kawamba ni janga la Kitaifa kwa sasa, hivyo ni lazima aondoke ndani ya wiki mbili, vinginevyo Chadema itaitisha maandamano makubwa nchi nzima kushinikiza kiongozi huyo ang'oke madarakani.

Hapa Mh. Mbowe alilia sanjari na wananchi waliojitokeza viwanja vya furahisha jijini Mwanza kilio kikielekezwa kwa wanafunzi wa kidato cha 4 waliofeli. |
"Kwa vile Waziri Kawambwa ameonekana kushindwa kuisimamia vema sekta hii ya Elimu, na kwa vile watoto wetu wengi wanafeli na kuishia kuandika matusi kwenye mitihani yao, Chadema tunampa wiki mbili awe amejiuzulu. "Kila mwaka, wanafunzi 1,200,000 hadi 1,300,000 wanafunzi nchi nzima wanafanya mitihani yao. Lakini wanaoshinda ni kati ya 35,000 hadi 400,000 pekee, hivyo watoto wengine wanashindwa kuendelea na masomo yao. Kwa hiyo huyu Waziri Kawambwa na Naibu wake tunataka wajiuzulu ndani ya wiki mbili", alisema Mbowe.
Alisema, kwa sasa Tanzania inazalisha vijana wapatao 800,000 kwa mwaka ambao wanakosa fursa ya kuendelea na masomo yao, na alimtaka Rais Jakaya Kikwete kuacha kucheka na kubembeleza viongozi wabovu wanaodidimiza maendeleo ya nchi na raia wake, na kwamba Tanzania inakabiliwa na majanga makubwa mawili ya elimu duni na udini.
Kuhusu Bunge kutooneshwa 'live', Mbowe alimuonya Spika Anne Makinda na wasaidizi wake kuacha kutumia madaraka yao kuwanyima uhuru na haki zao wananchi, na kwamba Watanzania wanahitaji kuwaona wabunge wao wabovu na wazuri ili mwaka 2015 wafanye maamuzi magumu ya kutokuwachagua ama kuwachagua tena.
"Makinda tumemwambia aache ubabaishaji katika uendeshaji wa Bunge. Watanzania wanataka kuwaona wabunge wao wanaolala, wanaoshangilia hoja za ovyo!. Tunataka Bunge liendeshwe kwa mazingira yanayomwezesha mwananchi kufahamu kila kitu kinachojadiliwa katika chombo hicho.
Akizungumzia maamuzi ya Chadema kuanzia uongozi wa kikanda, mwenyekiti Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Hai, alisema sera ya majimbo ni nguzo kubwa katika kuleta maendeleo kwa wananchi, hivyo chama chake hakijakosea kufanya hivyo na wanahitaji Tanzania igawanywe katika uongozi kwa ngazi ya majimbo ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo.
Alisema, licha ya kwamba sera yao hiyo inabezwa na CCM, lakini ndiyo mkombozi mkubwa katika adha ya umasikini miongoni mwa wananchi, hivyo wataisimamia kikamilifu kuanzia sasa na baada ya kuingia Ikulu katika uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015.
Katikati ya jiji mkutano umemalizika. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.