ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 21, 2013

MAANDALIZI KOMBE LA DUNIA KWA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU YAANZA NCHINI, SAFARI HII KIKOSI CHA TAIFA CHA WATOTO WA MITAANI KUSAKWA MIKOA YA DAR, ARUSHA NA MWANZA


Tizama video hii ujionee moja kati ya vituo hapa nazungumzia kituo cha Kuleana Mwanza.


NA. ALBERT G. SENGO: MWANZA

Maandalizi kwa mashindano ya Kombe la dunia kwa watoto wa mitaani yanatarajiwa kufanyika mnamo mwezi machi 2014 nchini Brazil yameanza rasmi hapa nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kituo cha malezi ya watoto waishio mazingira magumu cha TSC cha jijini Mwanza, Mutani Wangwe amesema kuwa hatua ya awali kwa maandalizi ya kuelekea Brazil, kituo chake kwa kushirikiana na wadau wengine wa soka kimeandaa mashindano yatafanyika kwenye miji mitatu maarufu hapa nchini ya Dar es salaam, Mwanza na Arusha, yakishirikisha watoto wa vituo vilivyoko kwenye miji husika ambapo vijana wa mikoa hiyo watashiriki kupata timu za mikoa na hatimaye timu hizo zitafanya ligi kwa ajili ya kupata timu ya Taifa ya Tanzania kwa Watoto waishio mazingira magumu itakayo kwenda nchini Brazil.

Zaidi huyu hapa mutani Yangwe Msikilize kwa kubofya HAPA....

Katika kufanikisha hili kwenye hatua za awali Premium League ya Uingereza imetoa kiasi cha paundi 15,000 ikihusisha gharama za safari ya wakufunzi wao watakaokuja hapa nchini.

Udhamini wa Ligi kuu ya nchini Uingereza kupitia vilabu vyake kwa soka la watoto wa mitaani umekuja kwa nia ya kujitanua zaidi Barani Afrika hivyo kwa kitendo cha kuchangia miradi kama hii ni promosheni tosha kwa Premeum League kuzidi kutanuka na kupendwa zaidi Ulimwenguni. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.