JANA KATIKA JAHAZI.
Mahakama ya wilayani Bunda mkoani Mara mnamo tarehe 17 jan 2013 ilimuhukumu kwenda jela miaka 3 raia wa china Mark Wang Wei (30) baada ya kukiri kosa la kutaka kutoa rushwa ya shilingi laki 5 kwa Mkuu wa wilaya hiyo Joshua Mirumbe.
Watangazaji wa kipindi cha Jahazi ndani ya Clouds Fm Ephrahim Kibonde (L) na Wasiwasi Mwabulambo (R) bOFYA kusikiliza... |
Mwanasheria wa Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) Mwema Mella aliiambia mahakama kuwa Wei alitenda kosa hilo jan 16 mwaka huu saa saba mchana katika ofisi ya mkuu huyo wa wilaya.
Mella alisema mshatakiwa ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Panda Internatinal Company LTD ya mjini Shinyanga, inayojihusisha na usambazaji wa pembejeo za kilimo, aliamua kufanya hivyo ili kumshawishi mkuu huyo wa ili ampitishe katika zabuni ya usambazaji wa pembejeo aliyokuwa ameiomba wilayani humo.
Alisema hata hivyo baada ya kubaini kuwepo kwa mazingira ya rusha katika mazungumzo kati yake na wei, Mirumbe aliamua kuwaita maofisa wa TAKUKURU waliofika mara moja na kuweka mtego uliofanikisha kumnasa mzabuni huyo na kufikishwa mahakamani.
Katika kujitetea kwake Wei aliyekuwa akitumia lugha ya kiingereza kwa taabu kwa kuwa haijui vizuri na mahakama haina mkalimani wa lugha ya kichina alisema hakujua kuwa kufanya hivyo kwa umpendaye ni makosa hapa nchini.
Alisema hilo ni tofauti na kwao ambako wanaliona tendo hilo kama la kawaida na kuiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu.
Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo Safina Semfukwe aliyeonekana kuguswa na maneno ya Wei, alisema kisheria kutokujua sheria hakumuondoi mtu yeyote hatiani hivyo alimhukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi laki 7.
Hata hivyo wei alilipa faini hiyo hivyo kujiepusha na kifungo hicho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.