ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 19, 2013

PALE VIJANA WAWILI WALIO VIONGOZI KAMBI TOFAUTI WANAPOTOA SOMO LA KUELEWEKA KWA WANANCHI

MEYA wa Jiji la Mwanza(Nyamagana) Bw.Stanislaus Mabula ambaye ni diwani wa kata ya Mkolani (CCM) amewataka Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata kushirikiana na Madiwani wao katika kupanga mikakati ya maendeleo na kuitekeleza kwa vitendo huku wakiwahamasisha wananchi kuchangia miradi ya maendeleo inayotoa huduma za kijamii badala ya kukalia malumbano yasiyokuwa na tija kwa wananchi kutokana na kuendeleza itikadi zao za vyama vya kisiasa zilizopo.

Wananchi wa Kata ya Igoma kusanyikoni.

Bw.Mabula alisema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Igoma wakati alipofanya mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya soko la wazi kwa lengo la kupatiwa taarifa za maendeleo za Kata hiyo pamoja na kukagua miradi ya kijamii iliyopo kwenye Kata hiyo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji, serikali kuu na wananchi kuchangia alisema kwamba wananchi wanao wawakilishi kuanzia ngazi ya Mitaa na Kata ili kero zao zitafutiwe ufumbuzi kwa kuwashirikisha wataalamu.
“Ni vyema wenyeviti, madiwani, watendaji na wataalamu kuwapatia taarifa za vikao vya WDC juu ya uamuzi wao na kuwaeleza wananchi jinsi ufumbuzi wa kero zinazowasumbua kwenye maeneo yao zilivyowasilishwa kwa Diwani ili kuhakikisha zinafikishwa kwenye Kamati za kudumu na Baraza la Madiwani kuzitafutia ufumbuzi wa haraka ikiwemo kuwaelekeza wataalamu kuzishughulikia kulingana na ilivyoamuliwa na kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza”alisema
Jeshi la Polisi wilaya ya Nyamagana nao walipata nafasi fupi ya kutoa somo kwa wananchi juu ya utii wa sheria, kujikinga, kukabiliana na uhalifu, jinsi ya kushughulikia kesi ndogondogo za majirani na jinsi ya kuzuia machafuko mitaani na majumbani. 
Awali diwani wa kata hiyo ya Igoma, Mhe. Adam Chagulani aliwataka wenyeviti kupeleka kwenye kikao cha WDC kero ambazo zimekuwa zikikwamisha utekelezwaji wa miradi ya maendeleo na ukwamishaji wa kukamilika kwake kwa kuweka kado ubinasifi na itikadi za vyama vya siasa wanavyotoka bali kwa kuzingatia masilahi ya wananchi waliowachagua kuwepo kwenye nafasi hizo.

Mkutano ulipomalizika Meya wa Jiji la Mwanza(Nyamagana) Bw.Stanislaus Mabula akibebwa na wananchi wa kata ya Igoma wakimuunga mkono kwa kuwa ni kijana mwenzao sambamba na kuonyesha ukomavu wa siasa.

Bw.Stanislaus Mabula alibebwa hadi eneo la biashara ndogondogo za akinamama sokoni hapo ambapo alifanya maongezi ya mtu mmoja mmoja kisha akaondoka eneo la kusanyiko

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.