ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 22, 2013

BODABODA WAZUA VURUGU MWANZA POLISI WAVURUMISHA MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA WAANDAMANAJI


NA ALBERT G. SENGO:MWANZA

Vurugu zimetokea leo majira ya asubuhi na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Mwanza mara baada ya waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kuandamana na kuwafanyia vurugu askari wa usalama barabarani ambao walikuwa katika zoezi la ukaguzi wa pikipiki zinazofanya safari ndani ya jiji hilo.

Jeshi la polisi lililazimika kuvurumisha risasi za moto hewani pamoja na mabomu ya machozi ili kuwatawanya waendesha pikipiki hao waliokuwawakifanya vurugu wakikusanyika toka sehemu mbalimbali za jiji kulazimisha wakaguzi hao kuwaachia wenzao waliokamatwa kutokana na kuvunja sheria mbalimbali za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na wengine kukosa leseni na kukosa kofia mbili za usalama kwa mwendeshaji na abiria kama ilivyoagizwa.

Kamanda wa jeshi la polisi Mwanza, Everist Mangu anathibitisha kutokea kwa vurugu hizo na hapa anasimulia kisa na mkasa kwa tukio hilo. Bofya play kusikiliza.


Ilikuwa saka nikusake baina ya madereva wabishi wa pikipiki na askari wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza.


Gari la dolia likipita eneo la Mission kirumba jijini Mwanza kuhakiki hali ya usalama.


Askari wajeshi la polisi katika harakati ya kutawanya waandamanaji kwa njia ya mabomuya machozi eneo la Mission Makongoro Kirumba jijini Mwanza.


Hizi ni harakati za jeshi la polisi Mwanza kupakia pikipiki zilizonaswa kwenye doria.


Wanausalama barabarani kazini katika kuzibaini pikipiki zinazokiukataratibu na sheria za usalama barabarani.


Mmoja kati ya vijana walionaswa na jeshi la polisi kukiuka sheria na taratibu za usalama barabarani akiwa kwenye difenda ya polisi naye akiomba usaidizi kupitia simu yake ya mkononi kwa ndugu na jamaa haikufahamika maramoja kwambaaliachiwa au laa kwani kwa wale waliokutwa na makosa wengi walitozwa faini   na kisha kuendelea na kazi , lakini kwa wale waliosababisha vurugu rungu la sheria lawangoja.


Wana usalama kazini.


Machafuko.


Kufuatia vurugu hizo safari kwa vyombo vya usafiri vinavyopaki eneo la mwaloni na maeneo mengine zimeathirika kwa abiria wake kushindwa kufika maeneo husika kwa wakati kutokana na kufungwa kwa muda kwa barabara ya Makongoro.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. WANA SIASA WANAWADANGANYA TuONE KAMA CHADEMA AU CCM WATAKUJA KUWATOA .TANGU LINI POLICE WAKASHINDWA?TEND KWA MAWAZO YANGU WANGEVUNJWA MIGUU ILI WAJUE SHERIA IPO NA SERIKALI NAYO IPO
    MISSANA DHL BUKOBA

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.