ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 28, 2012

WARSHA YA MAAFISA KUTOKA VITUO VYA MIPAKANI KUHUSU USIMAMIZI WA MAZAO/BIDHAA ZITOKANAZO NA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA YAFANYIKA LEO JIJINI MWANZA

Naibu Katibu  Mkuu Ofisi ya makamu wa Rais Eng. Ngosi C.X Mwihava akitoa hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya Maafisa kutoka Vituo vya mipakani kuhusu usimamizi wa Mazao / Bidhaa zitokanazo na Bioteknolojia ya kisasa inayofanyika leo La-Kairo Hotel Mwanza. 


Mwenyekiti wa Warsha hii Dkt. Julius Ningu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais akitoa maelezo kwa washiriki wa warsha ya Maafisa kutoka Vituo vya mipakani kuhusu usimamizi wa Mazao / Bidhaa zitokanazo na Bioteknolojia ya kisasa ambapo moja kati ya madhumuni ya warsha hiyo ni kukuza uelewa kwa maafisa wa mipakani (forodha/wakaguzi wa mazao/chakula na madawa) kuhusu usimamizi wa matumizi salama ya Biotekinolojia ya kisasa. 


Katika warsha hii washiriki wamepata fursa ya kukumbushwa majukumu yao muhimu kama yalivyoainishwa kwenye mfumo wa usimamizi wa mazingira dhidi ya athari zinazoweza kutokea kutokana na matumizi ya bioteknolojia ua kisasa hapa nchini. 


Vilevile Warsha hii pia ni fursa nzuri kwa washiriki kubadilishana uzoefu katika suala zima la usimamizi wa matumizi ya bioteknolojia ya kisasa hususani bidhaa au mazao ambayo yanaingizwa nchini kupitia katika mipaka yetu, bandari zetu na viwanja vya ndege.


Mtafiti wa Bioteknolojia nchini toka kituo cha Utafiti wa kilimo Mikocheni Dar es salaam Dr Emmarold E. Mneney akitoa darasa juu ya Kwanini Biotechnolojia ni muhimu kwa Tanzania. 


Washiriki takribani 30 kutoka katika wizara za kisekta na taasisi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na washiriki wa Wizara ya kilimo, Chakula na Ushirika Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC tawi la Mwanza, Mamlaka ya Chakula na Madawa TFDA tawi la mwanza, Taasisi ya Utafiti wa madawa ya Binadamu NIMR tawi la Mwanza wameshiriki Warsha hii.


Washiriki wengine ni Ofisi ya Forodha na zile za uthibiti wa mazao na mimea za mipaka ya Sirari, Mutukura, Kabanga na Ngara. 


Washiriki wengine ni Maafisa Afya wa mikoa ya kagera, mwanza, Shinyanga na Mara, washiriki wa kampuni za mbegu, mamlaka ya usimamizi wa mbegu (Tanzania Official Seed Certifying Institute -TOSCI) na bila kusahau wanahabari toka jijini Mwanza.

Naibu Katibu  Mkuu Ofisi ya makamu wa Rais Eng. Ngosi C.X Mwihava akizungumza na vyombo vya habari juu ya Warsha hiyo.. Msikilize kwa kubofya play.
Picha ya pamoja.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.