ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 9, 2012

HATIMAYE TRENI YA KWANZA YAWASILI MWANZA MARA BAADA YA KUSITISHWA SAFARI ZAKE MIAKA mi3 ILIYOPITA. ULANGUZI WAANZA, NAIBU WAZIRI ATOA AGIZO KUSIMAMISHWA MUHUSIKA DODOMA

Wakati leo Tanzania inasherehekea miaka 51 ya Uhuru wake, jiji la Mwanza linashuhudia safari ya treni ya kwanza ya abiria ikiwasili jijini hapa kutokea kituo cha kwanza jijini Dar es salaam,  tangu mara ya mwisho ilipositishwa takribani miaka mitatu iliyopita kutokana na wawekezaji waliopewa dhamana kipindi hicho kushindwa kuliendesha shirika la utoaji huduma hiyo.


Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk Charles Tizeba akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kwa maswali waliyokuwa wakiuliza sambamba na wananchi waliokuwa karibu kwenye kituo hiki cha reli jijini Mwanza hii leo kushuhudia kuwasili kwa treni hiyo ya abiria yenye mabehewa sita ya daraja la tatu na behewa moja kwa daraja la kwanza.


Treni ya Mwanza - Dar ilijengwa mnamo mwaka 1933 na Ujerumani enzi za ukoloni kwa madhumuni maalum ya kutoa huduma ya usafiri kwa njia ya reli kwa wakazi wote wa kanda ya ziwa hivyo kurejea kwa usafiri huu imekuwa suluhisho la adha ya usafiri na usafirishaji waliyokuwa wakipata wakazi wa kanda hii.


Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk Charles Tizeba ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi kuipokea treni hiyo alipata fursa ya kuzibainisha taratibu mbalimbali pamoja na Changamoto zilizopo... 
Bofya Play kuzisikia changamoto
Waandishi wa habari wakizinasa pointi... Kabla ya shirika la Reli nchini kubinafsishwa kulikuwa na safari za treni 4 zilizokuwa zikisafiri kwa kati ya Dar na Mwanza kila wiki,  lakini lakini TRC ilipobinafsishwa idadi ya safari za treni ilipungua hadi kufikia 2, na ilipofika 2009 mwezi disemba safari zikafutwa kabisa. 


Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Kondisaga, ambaye amemkaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza kwa sasa naye alikuwa na yake ya msingi ya kusema kubwa ni kutoa angalizo kwa sababu zitakazo pelekea kufa kwa safari za reli kama urasimu ukipewa nafasi..
Bofya Play kuzisikia..

Ni mwisho wa safari na hapa abiria  akikusanya vyake kutoka kwenye chumba cha usafiri wa treni daraja la kwanza  kupitia treni ya abiria ya kwanza tangu kusitishwa kwa safari zake miaka mitatu iliyopita Dar to Mwanza.


Ubao kwa leo kama unavyosomeka.


Usafiri huu hautumiwi na watanzania pekee bali pia watalii kama mmoja wapo anavyoonekana akishuka..


Enzi za nyuma safari zilikuwa toka Dar hadi hapa jijini Mwanza hadi Bukoba hatimaye Kampala nchini Uganda kwa tiketi moja, lakini sasa itabidi wananchi wavute subira kupisha maboresho yanayoendelea ikiwa ni pamoja na kuongezwa kwa mabehewa ambayo bado yapo kwenye karakana yakifanyiwa ukarabati kwani matarajio ni kuongeza zaidi mabehewa kwa kila daraja zaidi ya hapo. 


Korido za behewa daraja la Kwanza.


Ujumbe wa wananchi nje ya eneo la kituo...

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.