MUSOMA.
MAMLAKA ya Majisafi na taka Manispaa ya Musoma mkoani wa Mara (MUWASA) imewashusha waandisha wa habari njiani waliokuwa katika ziara ya Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Dk.Eng.Binilith Mahenge kwa madai ya kisingizio cha ufinyo wa bajeti.
Baadhi ya Waandishi wa habari wa magezeti ya mbalimbali mkoani hapa wameshushwa katika eneo la ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Manispaa ya Musoma na Afisa Mahusiano wa Mamlaka hiyo Emmanuel Ruyobya hali ambayo ni imeonekana kuwa ni udhalilishaji.
“Kiukweli huu ni udhalilishaji kwani sisi tuna vyombo vyetu ambavyo tunavifanyia kazi na si lazima tulipwe posho sasa huyu yeye anasema bajeti finyu wakati sisi hatujaomba posho” alisema mmoja wa waandishi wa habari walioshushwa katika gari hiyo.
Akisoma taarifa ya Maendeleo na Changamoto zake katika ofisi ya mkuu wa mkoa kwa Naibu,Katibu Tawala wa mkoa hupo Climent Lujaji alimuagiza mkurugenzi wa MUWASA Genes Kaduri kuwaweza waandishi hao katika suala la usafiri ili waweze kushiriki katika ziara hiyo ambapo mkurugenzi huyo alimkubalia .
Aidha Baada ya kuondoka katika eneo la ofisi wa mkoa waandishi wa habari hao walishishwa katika gari hiyo kwa madai hayo na kwamba wameishaalika waandishi wao .
“Kama Katibu Tawala wa mkoa ndiye kawaambia muje nendeni awalipe na kuwatafutia usafiri.,alisema Afisa mahusiano Ruyobya kwa jaziba kubwa.
Tabia ya kuwashusha waandishi wa habari si la mara ya kwanza katika ziara mbalimbali zinazofanywa na viongozi kama hao mkoani hapa hususani katika vyombo habari vya magazeti kubaguliwa na hata hivi karibuni 5 Oktoba mwaka huu imefanyika ziara ya Naibu waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele ambapo pia vyombo vingine vimebaguliwa.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Binilith Mahenge ameaza ziara yake ya kujua maendeleo na changamoto zake mkoa wa Mara ambapo imeanzia katika halmashauri ya wilaya ya Manispaa ya Musoma,Butiama kukagua chanzo cha maji cha Mugango –Kiabakari, Rorya,Serengeti na kumalizia wilaya ya Bunda.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.