ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 26, 2012

WATANZANIA WAASWA KUWA NA UZALENDO KAMA BABA WA TAIFA, WALIOTIMULIWA CCM, CHADEMA NA VYAMA VINGINE MILANGO IKO WAZI TADEA.

 Katibu Mkuu wa Tadea Taifa Bw. Juma Ally Khatibu akionyesha Kadi ya chama hicho yenye rangi 3, Blue ikiwakilisha Maji, Mito, Maziwa na Bahari,
Njano ikiwakilisha Madini.
Nyeusi ikiwakilisha sisi Waafrika.
Pia kuna nembo ya Mama na Mtoto kuonyesha kujali familia. 
Sikiliza kilichosemwa na uongozi huo kwa kubofya play.
Viongozi wa chama cha Tadea kutoka kushoto ni Tiba Deus katibu wa Tadea Mkoa wa Mwanza, Richar Gagi Mwenyekiti wa Tadea Mkoa wa Mwanza, Juma Ally Khatibu Katibu Mkuu wa Tadea Taifa na Charles Dotto Lubala Naibu katibu Mwenezi wa Taifa wa chama cha Tadea katika mkutano na waandishi wa habari.

 Waandishi wa habari ndani ya mkutano huo wa TADEA.

 Waandishi wa habari kazini...


 Watanzania wameombwa kuwa wazalendo na kuacha ubinafsi kama alivyokuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Mwalimu J. K. Nyerere ili kuweza kulinda rasilmali ya nchi yetu na ya vizazi vijavyo maana baadhi ya viongozi waliopo madarakani si wazalendo na hivyo kupelekea upotevu wa rasilmali kubwa za nchi ya Tanzania.

 Rai hiyo imetolewa leo na Katibu wa Chama cha The Tanzania Democratic Alliance TADEA Taifa Juma Ally Khatibu katika mkutano na waandishi wa habari leo kuhusu kampeni walinayo ya kuimarisha chama chao Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla ili kizidi kukubalika na kupendwa zaidi na wananchi wa rika yote.

 Amesema kuwa chama cha Tadea kimejipanga kusimamisha wagombea wa ngazi za kata 29 Tanzania na kila Mgombea atatumia shilingi Millini 3 na kufanya jumla yake kuwa Milioni themanini na saba.

 Viomgozi hao wamesema kuwa TADEA imejipanga kusimamisha wagombea ubunge na Urais katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015.

 Aidha amesema kuwa ili kuepusha maafa ambayo yanaweza kutokea kama katika nchi za Libya, Tunisia Misri na nyingine ambazo zimekosa amani, ni jukumu la Watanzania kuwa makini ya baadhi ya Vyama Vya kisiasa vinavyoiga matendo maovu ya nchi za Magharibi katika siasa.

Katika hatua nyingine kwa Chama hicho kujiimarisha kimefungua milango kwa viongozi wa vyama vingine vyote waliofukuzwa na vyama vyao iwe kanda ya ziwa au nchi kwa ujumla (vuta subira sauti itasikika). 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.