Mbunge wa viti maalum kupitia vijana (CCM) Mh Ester Bulaya ameendelea kutekeleza ahadi yake ya kugawa vifaa vya michezo katika Jumuiya za Vijana wa Chama hicho Mkoani Mara baada ya leo kugawa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 7.5 katika kata 34 kwa vijana wa Wilaya mpya ya Butiama mkoani Mara
Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Chama cha Mapinduzi Mkoani humo,Bulaya alisema kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo katika michezo atahakikisha yale aliyoyakusudia katika kutimiza azima yake hiyo anayatekeleza kadri atakavyoweza ili kila kijana katika Mkoa wa Mara aweze kushiriki katika michezo.
Chanzo www.mwanawaafrika.blogspot.com
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.