|
Naibu Waziri Ummy Mwalimu akicheza muziki wakati akiingia katika ukumbi
wa Yatch club Mwanza jana. |
|
Hapa wakimkabidhi zawadi kutoka kwa Mikaela Gateway Agency.
|
|
Inspector Modesta Masatu kushoto akiwa na Assistance Inspector Joyce
Kotecha moja kati ya walimu waliyotoa mada katika kongamano hilo. |
|
Kwaitoooo ikanoga ile mbaya kama inavyoonekana pichani.
|
|
Hapa Naibu Waziri akisaini daftari la wageni. |
|
Kina mama wanaweza wakiwezesha hapa kila mmoja akicheza kwa staili yake. |
|
Naibu waziri Ummy Mwalimu akifungua kongamano la kina mama. |
|
Sehemu ya kusanyiko hilo la akina mama
|
|
Akina mama wakibadilishana mawili matatu... |
|
Nisehemu ya kujuana pia.. |
|
Ni sehemu ya kumwaga furaha.... |
|
Pia kujifunza akina mama.. |
Wanawake wametakiwa kuisha kwa Malengo katika maisha yao na
kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa kutokana na changamoto mbalimbali
zinazowakabili kila siku.
Rai hiyo imetolewa jana na naibu waziri wa Maendeleo jinsia na
watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akifungua kongamano la kina mama 2012 jijini
Mwanza lililoandaliwa na Mikaela Gateway Agency ya jijini Mwanza ambalo
limewaleta kina mama wengi kutoka maeneo mbalimbali.
Mhe. Mwalimu amesema wanawake ni watu wa muhimu sana katika jamii
na kwa kulitambua hilo ndo maana Kongamano kama hilo likafanyika kwa kina mama.
Wanawake kutoka jijini Mwanza na maeneo mbalimbali ya Kanda ya
Ziwa wamejitokeza na kuhudhuria semina hiyo ambayo ni ya kwanza kufanyika
maeneo ya Kanda ya Ziwa.
Wanawake wamefundishwa mada mbalimbali kutoka kwa waalimu
walioandaliwa kama vile vile Mazingira, Ujasiliamali, Mawasiliano, Unyanyasaji
na ukatili wa kijinsia na utii wa sheria bila shuruti na Mahusiano.
Waandaaji wa kongamano hilo Mikaela Gateway Agency wamesema kuwa
huu ni mwanzo tu wa makongamano watakayoyaanda na watazidi kufanya hivi kila
mara siku wapatapo nafasi.
Baadhi ya washiriki wa
kongamano hilo wamefurahia masomo mbalimbali na kuonyesha na kutoa wito kwa
kina mama ambao hawakufika mara nyingine wasikiapo matangazo wajitokeze kwa
wingi.
Picha na F.pluss
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.