|
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza akifungua mashindano hayo, kushoto ni meneja wa bia ya Safari Oscar Shelukindo, mgeni rasmi akifuatiwa na katibu wa Chama cha Pool Taifa Amos Kafyonga, Kamanda wa Polisi Ilemela Debora Magiligimba |
Vijana wameaswa kujiepusha kutumia michezo kama sehemu ya uendeshaji wa biashara haramu na mipango ya matendo maovu kwa jamii ili kuleta maana halisi ya kuwa Michezo ni Afya, Michezo ni Ajira.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Amina Masenza ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Safari Pool Taifa ambapo jiji la Mwanza kwa mwaka huu 2012 limepewa hadhi ya kuwa wenyeji.
"Baadhi ya maeneo wamegeuza mchezo wa Pool kuwa eneo la 'Mishenitaun' (eneo ambalo mipango ya uhalifu inafanyika) lakini la pili ni sehemu ya mauzo na usambazaji wa madawa ya kulevya, ni eneo la ugomvi, ni eneo la majigambo yasiyokuwa na faida kwa jamii na maisha vilevile eneo la wasiotaka kufanya kazi ambao wamegeuza kaya yao ya kudumu" Alisema Mkuu wa wilaya ya ilemela Mhe. Masenza.
Kisha akaongeza kuwa.. "Ni eneo ambalo utakuta lugha chafu na kadhalika, hayo siyo mambo mazuri ya kutambulisha kuendeleza mchezo wa pool hivyo wekeni mikakati ya kuyakataa na kuyadhibiti kama Chama na kama Wachezaji, kama Viongozi na kama Watanzania, kwani hayo hayatatujenga bali kutuangamiza na kupoteza dira ya mchezo husika"
|
Timu kutoka vilabu vya mikoa mbalimbali ziko jijini Mwanza kwaajili ya ushiriki michuano hiyo ndani ya ukumbi mkubwa wa Monarch Hotel & Pavillion. |
|
Ni moja kati ya timu husika na Mashindano hayo. |
|
Kamanda wa Polisi Ilemela Debora Magiligimba sambamba na kuwahakikishia usalama washiriki hao pia hakusita kuwaasa akisema kuwa "Siyo kwamba Ukimwi Mwanza haupo, upo ila umejificha na utaupata ukiutafuta." ambapo wengi waliangua kicheko kwa kauli hiyo yenye mtego... |
|
Jumla ya timu 16 zinashiriki Safari Pool Taifa 2012 ambapo jijini Mwanza ndiyo waandaaji. |
|
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza akifungua mashindano hayo kwa kulenga...... |
|
Hureeeeee....!!!!! |
|
Mara baada ya uzinduzi huo makepteni wa timu zote waliikaribia meza kwaajili ya kupiga kura kujua timu zipi wataanza nazo. |
|
Akina dada hawa nao ni sehemu ya wachezaji timu mbalimbali. |
|
Kwa mujibu wa Oscar Shelukindo ambaye ni meneja wa bia ya Safari wadhamini wa michuano hiyo amesema kuwa Timu Bingwa wa Michuano hiyo inayoshirikisha timu 16 ataondoka na pesa taslimu shilingi milioni 5, kombe na medali ya dhahabu. Washindi wa pili kunyakuwa milioni 2 na laki 5, Washindi wa tatu kunyakuwa shilingi milioni 1 laki 2 na nusu. Washindi wa nne shilingi laki 7 kibindoni. Kisha zawadi nyingine kibao kwa washiriki pool mmoja mmoja. |
|
Mbele ni waamuzi na nyuma ni wachezaji wa Michuano ya Safari Pool Taifa yaliyozinduliwa leo Monarch Hotel, Ilemela jijini Mwanza. |
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.