Kipindi cha The Big Top Ten, Star TV, kitaanza tena kuruka Live siku za Jumanne saa 5 usiku baada ya hapo awali kurushwa kila siku za ijumaa saa 6:40 mchana.
Mabadiliko hayo yamefanyika kufuatia wapenzi wengi wa muziki wa kizazi kipya, kutoa maoni yao juu ya kipindi hicho kufanyika LIVE tena usiku.
The Big Top Ten ni kipindi kinachorushwa kupitia Star TV, kikiwa na maudhui ya kurusha hewani video kumi zenye ubora wa hali ya juu katika mpangilio wa kuanzia nafasi ya Kumi hadi ya Kwanza.
Katika Video bora The Big Top Ten inaangalia Mpangilio wa picha, Mpangilio wa Midundo (Beats) na Mpangilio wa Mashairi.
The Big Top Ten pia hutoa mada katika kuendeleza wa muziki wa kizazi kipya, ambapo watazamaji huchangia kwa kupiga simu LIVE Studio, katika ukurasa wetu wa Facebook na kwa kutuma Ujumbe mfupi.
Mtanzania ni wakati sasa wa kuthamini cha kwetu kwa kutoa mchango wako wa hali na mali katika kuuendeleza muziki wa kizazi kipya uwe katika next level.
Nategemea ushirikiano wako katika The Big Top Ten kila siku za jumanne saa 5 usiku LIVE. Kuanzia Jumanne hii!!
TUKUTANE BASI WAKATI HUO.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.