ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, September 30, 2012

ILALA YAIADHIBU VIKALI KINONDONI NA KUTWAA SAFARI LAGER POOL TAIFA 2012: MBEYA YATAMBA WASHIRIKI SINGLE

Mabingwa wa Safari Lager Pool Taifa 2012 Kayumba toka Ilala jijini Dar es salaam wakisherehekea na kombe lao mara baada ya kuigagadua Meeda ya Kinondoni kwenye fainali iliyofanyika leo katika ukumbi mkubwa wa Hotel Monarch jijini Mwanza. 

Bingwa wa medali ya dhahabu na kitita cha shilingi 800,000/= katika single pool wanawake Ted Sanga kutoka mkoani Mbeya akichuana kwenye fainali na mshiriki kutoka mkoani Kilimanjaro Secilia Kileo aliyenyakuwa medali ya fedha na kitita cha shilingi 350,000/= 

Mshabiki wamevutiwa na ubora ulioonyeshwa na waandaaji wa michuano ya Safari Lager Pool Taifa 2012 jijini Mwanza hali inayoufanya mchezo huo kuthaminika na kupata hadhi ya juu kinadharia na vitendo.

Mmoja kati ya wachezaji wakali waliyoiongoza Kayumba 'Yeyo' Ilala kutwaa ubingwa akisukuma ball kwa shimo kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Meeda ya toka Kinondoni zote za jiji la Dar es salaam.
Msahabiki wakifuatilia fainali hizo.


Bingwa wa Single Pool Wanaume Solomon Elias kutoka mkoani Mbeya akipokea kombe la ubingwa na fedha taslimu shilingi 500,000/= toka kwa mgeni rasmi.

Bingwa wa Single Pool Wanaume Solomon Elias kutoka mkoani Mbeya ambaye anaulemavu wa kutoongea (bubu) akipata flash na mashabiki wake jijini Mwanza 

Washindi wa pili kwa upande wa timu, Meeda ya Kinondoni licha ya kupata medali ya Fedha walivuna kitita cha shilingi 2,500,000/= 

Mabingwa wa Safari Lager Pool Taifa 2012 Kayumba toka Ilala jijini Dar es salaam wamevuna kitita cha shilingi 5,000,000/=

Mabingwa wa Safari Lager Pool Taifa 2012 Kayumba 'Yeyo' toka Ilala jijini Dar es salaam wakisherehekea na kombe lao mara baada ya kuigagadua Meeda ya Kinondoni kwenye fainali iliyofanyika leo katika ukumbi mkubwa wa Hotel Monarch jijini Mwanza. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.