Mwenyekiti mpya wa IDFA Evarist Hagira akikabidhiwa katiba ya Chama cha soka Wilaya ya Ilemela na mwenyekiti wa uchaguzi Japhet Mbwana baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo. |
Mwenyekiti wa MZFA mkoa wa Mwanza Jackson Songora akitoa nasaha kwa wajumbe wa vilabu vya soka wilaya ya Ilemela kabla ya wagombea kujinadi. |
Jackson Songora na wajumbe. |
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Yusuph Juma akitoa maelezo juu ya Taratibu za uchaguzi wilaya ya Ilemela. |
Mwenyekiti wa uchaguzi huo Japhet Mbwana akitiririka juu ya taratibu za uchaguzi. |
Katibu MZFA Nasibu Mabrouk akitoa yake machache mbele ya mkutano huo wa uchaguzi wilaya ya Ilemela. |
Na Albert G. Sengo: Mwanza
CHAMA cha mpira wa miguu Wilaya ya Ilemela (IDFA) jana kilifanya uchaguzi wake mdogo wa kuziba nafasi ya Mwenyekiti ambaye ilikuwa wazi tangu aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa March 31 mwaka huu Lazaro Nduta, kupigiwa kura nyingi za hapana na kuondoshwa madarakani.
Uchaguzi huu ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa chuo cha Maliasili eneo la Pasiansi wilayani Ilemela jijini Mwanza ambapo wagombea wawili wa nafasi hiyo Evarist Hagira na Frankline Kamalamo wote walijinadi kwa Wajumbe 113 kabla ya kupigiwa kura.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi huo Japhet Mbwana amesema kuwa kolamu ya wajumbe hao kutoka vilabu vyote vya wilaya ya Ilemela ilikuwa inaruhusu kufanyika kwa uchaguzi huo.
Akitangaza matokea hayo Mwenyekiti wa Uchaguzi huo Mbwana alisema kuwa jumla ya wajumbe 113 wamehudhuria na kura zilizopigwa ni 113 kura 9 ziliharibika Hagira akipata ushindi kwa kupata kura 79 dhidi ya 23 alizopata Kamalamo hivyo kwa mujibu wa katiba ya TFF. Hagira akatangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti chama cha mpira wa miguu wilaya ya Ilemela.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.