| Bibi Veronica Stima akimvalisha mumewe Allen. |
| Wakiwa katika nyuso za tabasamu zito ni Bwana na Bibi Allen Munene. |
| Padre Kalaso (kati) wa Kanisa la Familia Takatifu Parokia ya Ipuli, Tabora akimuelekeza Bwana Allen Munene kutia saini katika cheti huku pembeni yake mkewe Veronica akishudia. |
| Nae mkewe akitia saini. |
| Wakiwa katika nyuso za furaha na kuonyesha vyeti vyao. |
| Pongezi nyingi zikiwamiminikia Bwana na Bibi Allen mara baada ya kufunga pingu za maisha. |
| Mama mzazi wa Bibi harusi akitoa baraka zake za pekee kwa mwanae mpya wa kiume ambaye ameungana na mwanae. |
| Pozi la pekee; bibi harusi akiwa na wasimamizi wake. |
| ...Maharusi wakiingia ukumbini kwa furaha. |
| ...wakishangiliwa mara baada ya kukata utepe na kuingia ndani ya ukumbi. |
| ...wapambe nao wakiingia kwa madaha. |
| Bibi Veronica akigawa shampeni kwa wakwe zake. |
| Nae bwana Allen Munene akigawa shampeni upande wa wakwe zake. |
| ...Tunywe kwa afya na maisha yetu... |
| Wapendanao wakikata keki kuonyesha umoja na upendo kati yao. |
| Maharusi wakigawa keki upande wa Mzee Munene. |
| ...Huku nako Baba na Mama Stima wakipokea keki kutoka kwa watoto wao. |
| ...nderemo na vifijo vilitawala ukumbini... |
| Wachanga na ile staili yao ya kushikana mikono, kudumisha umoja na mshikamano kati yao. |
| ... Upendo na mshikamano udumu milele. |
| Wapare nao hawakuwa nyuma na staili yao ile ya kuwema mikono nyuma... |
| Wafipa sasa wao walikuja kisasa kabisa... |
| ...huku nako mambo ya pwani yaliendelea kunoga... |
| ... Ni bwana Cathbert Angelo mmiliki wa CEO wa www.kajunason.blogspot.com akiwa na mama na baba zao (wakwe). Mavazi ya Bwana na Bibi Allen Munene yamebuniwa mbunifu wa mavazi Manju Msita. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment