ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, August 5, 2012

DHULU SPORTS CLUB YATOA ELIMU YA AFYA JUU YA UKIMWI NA MADAWA YA KULEVYA KWA SHULE YA SEKONDARI BUGARIKA

Mwenyekiti wa Dhulu Sports Club Habibu Hassan (Binya) akionyesha bango la mkakati wa klabu hiyo ya michezo ililotundikwa katika shule ya sekondari Bugarika jijini Mwanza, Dhulu club ni Kilabu ya michezo mbalimbali hususani mpira wa miguu kwa vijana wa jinsia zote yenye lengo la kutoa elimu ya afya kupitia michezo.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Bugarika wakisoma bango la club yenye kujihusisha na michezo kama mpira wa miguu, pete, kikapu, volleyball, tennis, ngumi n.k.

Mwenyekiti wa Dhulu Sports Club Habibu Hassan (Binya) akitoa darasa kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Bugarika juu ya jinsi kijana anawezaje kujikinga na ulevi, uvutaji bangi, madawa ya kulevya, uporaji na kuepuka ugonjwa wa ukimwi ambao umeathiri vijana wengi hapa nchini.

Mwenyekiti wa Dhulu Sports Club Habibu Hassan (Binya) akitoa mwongozo kwa Head girl wa Bugarika Sec na kulia mwisho ni Head boy wa shule hiyo ile hali wa pili kutoka kushoto ni katibu wa klabu hiyo Donard Julius (Don)

Moja kati ya sifa za uanachama kwa klabu hiyo ni Kijana awe na akili timamu, awe na umri kati ya miaka 7 na kuendelea, awe na uwezo wa kuelewa na kutambua haki na wajibu wake katika club, hii itaepusha migogoro na usumbufu ndani na nje ya club... na mengineyo.

Ni mengi yenye manufaa kwa vijana yalijadiliwa hapa bila kusahau nafasi kwa wanafunzi kuuliza maswali pamoja na kuchangia mawazo.

Engo ya chini ya mti na wanafunzi wa shule ya sekondari Bugarika Mwanza.

Somo likiendelea mada iliyogusa wengi ni kuhusu suala la ugonjwa wa ukimwi...
Hongera Bugarika Sec kushiriki zoezi hilo next time tutahamia shule ya sekondari Buhongwa endelea kufuatilia hapa hapa bloguni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.