Askofu wa Kanda ya Ziwa Victoria FGA Zenobius Isaya akizungumza na kusanyiko lililojitokeza kwenye uwanja wa nyamagana jijini Mwanza jana jioni. |
Baraza la makanisa ya Kipentekoste nchini Tanzania (CPCT) mkoa wa Mwanza kwa ushirikiano na jeshi la Polisi jana katika uwanja wa Nyamagana, wamefanya uzinduzi wa kampeni ya baraka na thawabu za utii bila shuruti katika mkoa wa Mwanza, kampeni yenye kusudi la kuzuia uhalifu kwa njia ya mahubiri.
Kampeni hiyo imekuja baada ya uzinduzi ule wa awali wa kitaifa uliofanyika tarehe 19/06/2012 katika jiji la Dar es salaam.
Kampeni hiyo imekuja baada ya uzinduzi ule wa awali wa kitaifa uliofanyika tarehe 19/06/2012 katika jiji la Dar es salaam.
Sehemu ya umati uliojitokeza kwenye viwanja vya Nyamagana Mwanza kwenye kusanyiko hilo lililogusia Amani ya nchi na umuhimu wake na mbinu gani zitumike kuwajenga watu kifikra.
Baadhi ya wahudhuriaji walioketi jukwaa kuu.
Tukio hilo la uzinduzi limehusisha wachungaji, maaskofu na waumini wa makanisa mbalimbali jijini Mwanza.
Mwananchi aliyejitokeza kuungama kujihusisha na vitendo vya uhalifu nakukiri kuwa imetosha sasa anamgeukia Mungu.
"Sisi kama watumishi wa Mungu tunaanza na gia ya kwanza ambayo ni maombi, yaani kupeleka hiyo shida kwa Mungu ili aingilie kati, 'Biblia inasema Yeye Mungu asipolinda wale walindao wanakesha bure', Mungu huwa anayaona na kuyasoma hata yale ambayo mwanadamu hayaoni, hatua ya pili huwa tunashauri serikali kwamba pamoja na serikali inapoendelea kuongoza sisi pia tuna macho ya kuona na tunaamini nasi kwa kibali cha kuitwa wananchi tunapaswa kutenda kazi za chini kuisaidia serikali ndiyo maana leo tumekusanyika hapa kuwalisha neno wananchi wetu juu ya suala zima la utii bila shuruti yaani utii bila kulazimishwa"
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.