Chama cha mapinduzi wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi waandamizi wilaya ya Ilemela leo kimefanya maandamano ya amani kwa lengo la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa tarehe 01/07/2012 iliyokuwa imejaa uwazi na ukweli kufuatia mgomo wa Madaktari nchini
Katika risala ya Chama hicho iliyowasilishwa na katibu wake Mwenezi wilaya ya Nyamagana Dr.Elirehema Moses Kaaya imewasihi Madaktari wote warudi kazini mara moja ili kuendelea kuwahudumia watanzania wanaoteseka na wanaohitaji huduma za afya hospitalini.
Dr. Kaaya amesema kuwa nikweli madai ya madaktari yana mantiki kubwa, hasa ukizingatia ugumu na mazingira wanayofanyia kazi, hata hivyo Serikali kwa kiwango kikubwa imejitahidi kutekeleza baadhi ya matakwa yao, hii ikiwa ni pamoja na kuwaondoa viongozi wakuu wa Wizara ya Afya, nyongeza ya mishahara na posho nyingine.
Chama hicho kimesema kuwa hakina ugomvi na madai hayo, bali tatizo ni njia ambayo Madaktari wameamua kutumia kudai madai yao hayo kwani wengi hupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa maisha.
Kupitia hadhara hiyo CCM Nyamagana imewasihi madaktari wote waliogoma kusitisha mgomo huo na kurejea kazini ili kuwahudumia na kuokoa maisha ya watanzania wanaoendelea kupoteza maisha na wakumbuke kuwa uhai wa binadamu hauwezi kuthaminishwa kwa fedha au kitu chochote hivyo utangulizwe utu kwanza.
Mabango ya wananchi na ujumbe.
Wana mupoooo...!!
Wananchi walioketi wakisikiliza yanayojiri huku wakiwa na mioyo ya matumaini kwamba madaktari wao ni weredi, wasikivu na wenye huruma hivyo watarejea kazini na kuendelea kuwahudumia.
Tunaomba kuwasilisha....!!
Washiriki wa Igizo lililofana kwa ujumbe wa kusisimua..
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.