ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 12, 2012

MWANAMKE ALIYEBURUZWA NA MUME UVUNGU WA GARI AFARIKI


Enzi za uhai wake akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza.
Na Mwandishi wa blogu hii
Shomari Binda
Musoma


Mwanamke mmoja wa Mjini Bunda Aisha Elias aliyeburuzwa uvunguni mwa gari kwa zaidi ya kilometa 50 na mume wake kwa kile kilichodaiwa ni wivu wa mapenzi amefariki dunia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amepelekwa kwa ajili ya kupata matibabu zaidi kutokana na majeraha aliyokuwa ameyapata.


Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho,kamanda wa Polisi Mkoani Mara Absalom Mwakyoma amesema kabla ya kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi hadi alipofikwa na mauti alikuwa akiugulia kwa muda katika hospitali ya rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.


Kamanda Mwakyoma amesema tukio la kuburuzwa uvunguni mwa gari kwa mwanamke huyo lilitokea Februari 2 mwaka huu majira ya saa moja jioni katika maeneo ya Yankiz barabara ya Nyerere mjini Bunda.


Ilidaiwa mume wa mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Elisha Endru Makumbati aliyekuwa na gari namba T 400 BBC aina ya nissan patro alimuita mke wake Aisha Elias kwa nia ya kutaka kumsalimia na kisha kumshika nguo na kuliondosha gari hilo kwa kasi na kudondokea uvunguni mwa gari na kuanza kuburuzwa.


Mwakyoma amesema jeshi la Polisi bado linaendelea kumtafuta Elisha Endru Makumbati aliyotoroka mara baada ya kufanya tukio hilo na pale atakapopataikana atafikishwa katika vyombo vya sheria ili aweze kujibu mashitaka yanayomkabili.


Aidha kamanda Mwakyoma ametoa wito kwa wananchi kutojichukulia maamuzi yasiyofaa katika jamii pale panapotokea kutokuelewana katika familia bali kuwepo na mazungumzo kutoka pande zote zinazokinzana yenye kufikia muafaka ili kuepusha matatizo ambayo yanaweza kujitokeza.


Amesema kujiingiza katika matatizo kama hayo kwa mume na mke kunapelekea familia kuishi katika maangaiko ikiwemo elimu isiyo na tija,chakula na masuala mbalimbali ya kijamii na kuzalisha watoto wanaodaiwa kuishi katika mazingira magumu na kudai kuwa matatizo ndani ya nyumba yanazungumzika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.