Na mwandishi wa blogu hii
Shomari Binda,
Musoma
Wanachama wa vyama vya siasa hapa nchini wametakiwa kuwa wavumilivu katika hoja za kisiasa ili kuweza kufanikisha dhana ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi na demokarasia ya kweli katika kufanikisha mfumo huo.
Kauli hiyo imetolewa na afisa mfawidhi wa katoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa hapa chini kutoka kanda ya ziwa lodovick Joseph wakati akisoma idadi ya watu walijitokeza kukidhamini chama kipya cha siasa hapa Nchini cha allance Democratic Change (ADC) katika ukumbi wa mikutano wa Musoma club.
Alisema wanachama wa vyama vya siasa wanapaswa kuwa wavumiliovu katika siasa ili kuendana na malengo ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi na uhuru wa mtu kwenda chama chochote cha siasa anachoona kinamfaa kujiunga nacho kutokana na sera zake na mfumo wake.
Lodovick alisema wapo baadhi ya wanachama wa vyama vyama vya siasa wasio wavumilivu katika siasa za kistaarabu na kupelekea kuanzishwa kwa vurugu zisizo za msingi na kusababisha madhara kwa jamii ikiwemo kusababisha usunbufu kwa wanachi wengine katika shughuli zao.
Alisema Mkoa wa Mara umevuka lengo la wanachama waliojitokeza kukidhamini chama cha (ADC) ambapo jumala ya wanachama waanzilishi 250 kutoka wilaya za Mkoa wa Mara walijitokeza kukidhamini na kuizidi mikoa ya Mwanza,Tanga na Pemba ambapo tayari chama hicho kimeshakwenda kutafuta wadhamini.
Akizungumza na wanachama wa chama hicho mara baada ya kutangazwa kuvuka lengo la wanachama waliojitokeza kukidhamini chama hicho,Kaimu Katibu mkuu wa chama cha ADC Kadawi Lucas Limbu aliwashukuru wanachama hao kwa kujitokeza kwa wingi na kuonyesha ni namna gani walivyo tayari kwa ajili kutaka mabadiliko.
Alisema lengo la kuanzishwa kwa chama hicho ni baada ya kuonekana vyama vingi vya kisiasa vilivyoanzishwa hapa nchini kushindwa kufikia malengo ya kuanzishwa kwake na kutokukidhi yale ambayo wananchi wanayatarajia kutoka katika vyama hivyo.
Limbu alidai viongozi wa vyama hivyo vya siasa katika ngazi ya Kitaifa wamekuwa wabinafsi na kushindwa kuwashirikisha viongozi wengine katika ngazi za chini katika wilaya hasa pale chama kinapopata mafanikio na kueleza kuwa chama Cha ADC kitakuwa mfano wa kuigwa katika kuwashirikisha wananchama wake na viongozi katika kada zote.
Iwapo chama cha ADC kitakamilisha masharti ya kuanzishwa kwa chama cha siasa hapa nchini waliyopewa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa hapa nchini kitakuwa chama cha siasa cha 20 tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.