ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 13, 2012

BONANZA LA TASWA ARUSHA KUTIMUA VUMBI JUMAPILI

 Katibu wa Chama cha mpira wa miguu mkoani Arusha (Taswa) Mussa Juma akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye hoteli ya Palace mjini humo juu ya bonanza la waandishi hao lililoandaliwa na kampuni ya MS Unique litakalofanyika kesho jumapili saa 2 asubuhi kwenye viwanja vya General Tyre vilivyopo Themi mjini humo,(kushoto) ni Mratibu wa bonanza hilo, Jamilah Omary na Meneja matukio wa kampuni ya bia nchini TBL wa kanda ya kaskazini,George Mwombeki ambao ndiyo wadhamini wakuu wa bonanza hilo.

Meneja matukio wa kampuni ya bia nchini TBL,George Mwombeki akizungumza na waandishi wa habari jana Palace hotel mjini Arusha kuhusiana na udhamini wa Bonanza la waandishi wa habari za michezo mkoani Arusha (Taswa) ambapo kampuni hiyo ndiyo wadhamini wakuu wa bonanza hilo lililoandaliwa na kampuni ya Ms Unique (kulia) ni Katibu wa Taswa mkoani humo Mussa Juma na kushoto ni Mratibu wa bonanza hilo Jamillah Omary.
Picha/Habari na Woinde Shizza,Arusha

BONANZA la Chama cha waandishi wa habari za michezo (Taswa) wa mkoa wa Arusha linatarajia kutimua vumbi jumapili hii kwenye viwanja vya General Tyre vilivyopo Themi mjini humo.

Mratibu wa Bonanza hilo,Jamilah Omary akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa Palace Hotel alisema mgeni rasmi wa bonanza hilo anatarajiwa kuwa mbunge wa viti maalum vijana wa mkoa huo Catherin Magige.

Jamilah alisema bonanza hilo limeandaliwa na kampuni ya Ms Unique na linafanyika kwa kipindi cha mwaka wa saba mfululizo likishirikisha mabingwa watetezi Radio 5,Radio Sun Rise,Triple A,ORS ya Manyara na Chuo cha uandishi wa habari cha Arusha (AJCT).

Naye,Katibu wa Taswa wa mkoa huo,Mussa Juma alisema bonanza la mwaka huu limeboreshwa zaidi ambapo bingwa wa michuano hiyo atazawadiwa Sh150,000 mshindi wa pili sh100,000 na timu yenye nidhamu sh50,000.

“Lengo la bonanza hili ni kuwakutanisha waandishi wa habari kwani michezo ni afya,burudani na kujenga undugu hivyo tunawataka waandishi wote wafike siku hiyo kwa ajili ya kufanikisha bonanza hili,” alisema Juma.


Timu zinazoshiriki ni Radio5,Radio Sun Rise,Triple A,ORS Radio ya Simamanjrio Wazee club kampuni ya bia kitambi nowa ya netiboli na chuo cha Arusha uandishi wa habari cha Arusha.

Wadhamini TBL inawafanya waweze kuandaa tamasha kila mwaka Tanapa kituo cha mikutano cha AICC,Mamlaka ya hifashi yang'ara NCCIA mfuko wa jamii ya NSSF Mega Trade wakala wa simu za mkononi Alphatel Palace Hotel

Mshindi wa kwanza kombe na 150,000 pili 100000 timu yengye nidhamu 50,000 Soka mbio za magunia,kuvuta kamba netiboli kukimbiza kuku mbio za magunia na taikondo


Kwa upande wake,Meneja matukio wa TBL Kanda ya kaskazini George Mwombeki meneja matukio wa TBL Kanda ya kaskazini masharini kuu wa idara ya matukio wa kampuni ya bia TBL Maandalizi ya mwaka huu yameanza vizuri kuliko mwaka uliopita na tunatarajia pia mkuu mpya wa wilay aya Arusha,John Mongela na vijana wa taikondo burudani mbalimbali Alisema sh25 milioni zimetumika katika kugharamia bonanza hilo la Taswa la mwaka huukatika mpambano huo tamasha la wanaa

“Waandishi wote wa habari mnatakiwa kuja na familia ze,” alisema Juma.

Mwombeki alisema kampuni yao ina thamini sana waandishi wa habari ndiyo sabau tunashiriki kudhamini Natoa wito kwa waandishi wote na wakazi wa mkoa huo kwani kutakuwa na vinywaji na nyama choma pamoja na burudani tofauti tofauti kwani kiingilio ni bure hivo wajitokeze kwa wingi.
MWISHO.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.