Warembo wa miss universe Tanzania 2012 wameanza rasmi kambi katika hoteli yenye hadhi ya kipekee Urban Rose Hotel. Hii ni kwaajili ya kujiandaa na fainali ya Miss Universe Tanzania 2012 itakayofanyika tarehe 29 mwezi huu wa juni.
Miss Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo
mbalimbali kwa ajili ya kuwapa warembo ili kujitambua kama vijana na kama
wanawake. Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali toka katika
nyanja tofauti ikiwemo TGNP.
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications
ambaye pia ni mkurugenzi na muandaaji mkuu wa kitaifa wa mashindano haya Maria
Sarungi Tsehai amesema kuwa tofauti na miaka ya nyuma mbali na kuongeza semina
zaidi ili kuwasaidia warembo lakini pia imefanikiwa kuongeza mikoa ambapo mwaka
huu wameshiriki warembo kutoka mikoa saba ya Tanzania.
Mbali na kutafuta warembo tu bali Miss Universe
ni kama chuo cha kufundisha warembo juu ya kujitambua kama mwanamke na kumpa
mbinu mbalimbali za kimaisha.Vilevile mbali na mshindi kupata nafasi ya kutembea
nchi mbalimbali za kimataifa pia hutoa fursa kwa mshindi kupata nafasi ya kwenda
kusoma nje ya nchi kama vile Marekani kwa kupitia mdhamini wetu mkuu New York
Film Academy’’
Kambi ya Miss universe Tanzania 2012
imekamilishwa na warembo 20 kutoka mikoa saba ya Tanzania ambayo ni
Dodoma, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Manyara, Mtwara na Dar es Salaam.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yalianza
rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye
mbali na kuliletea sifa taifa bali pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya
ulimbwende kwa kuwa mwanamitindo wa kimataifa. 2008 Miss Universe Tanzania
iliwakilishwa na Amanda Ole sululu, 2009 Illuminata James, 2010 Hellen Dausen na
Nelly Kamwelu ambaye ndiye anakabidhi taji kwa mshindi wa mwaka huu.
Mashindano
ya Miss Universe Tanzania yamedhaminiwa na Le Grande Casino, The citizen, Urban
Rose Hotel, Amina Designs, Dodoma Hotel na New York Film Academy
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.