ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 17, 2012

WAMILIKI WA VIWANDA WAINGIA MITINI KUKWEPA MKUTANO NA WAVUVI KUJADILI KUSHUKA KWA BEI YA SAMAKI


Video ya kilio cha wavuvi Mwanza kwa serikali kuwaundia Bodi ya Wavuvi itakayo husika kudhibiti bei ya zao la samaki kama ilivyo kwa zao la pamba, kahawa, korosho, vyombo vya usafiri majini na nchikavu kuwa na bodi zao.



Wamiliki wa viwanda vya kuchakata, kusindia na uuzaji nje samaki vilivyopo Mwanza, leo wameingia mitini wakikacha kuhudhuria mkutano baina yao na maajenti na wavuvi ambapo ulikuwa na lengo la kujadili anguko la sasa kwa bei ya samaki ambalo ndani yake linaonekana lina vimelea vya ujanja ujanja kunufaisha upande mmoja. Pichani ni meza ya Uongozi wa Chama cha Wavuvi Kanda ya Ziwa (TAFU). 


Mratibu wa Chama Cha Wavuvi Juvenile Matagire
Hata hivyo wavuvi hao wameendelea na mkutano wao na hatimaye kutoa maamuzi ambapo moja kati ya maazimio ni Kumwomba mkuu wa mkoa kupitia chama chao TAFU kuonana naye mara kwa mara kwaajili ya kujadili maendeleo na matatizo ya uvuvi na biashara ya samaki kwa ujumla kwani mara nyingi wamekuwa wakikumbana changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na dhuruma.


Wavuvi mkutanoni.
Wakiwa ndani ya mkataba wavuvi hao walishuhudia bei ya samaki ikishushwa kwa asilimia hamsini na kuathiri utendaji kazi wao na maisha ya jamii inayowazunguka pia wavuvi hao wameshangazwa kuona yote hayo yanatendeka ile hali waziri wa wizara husika hajui wala hana taarifa ya poromo hilo la bei.


"Ukiachana na tatizo hili la bei kuna mengine mengi yanayotukumba sisi wavuvi ndiyo maana hatuendelei mfano ninaleta samaki wangu wakiwa fresh kiwandani wanapoingia kufanyiwa uchakataji kwenye tani mbili au moja zinapatikana kilo 200 rejekti (kwamba samaki hawafai) hiyo rijekti badala urudishiwe inakwenda humo humo kiwandani kwenye hesabu unaandikiwa shilingi 300/=  kwa samaki wa kilo moja mwenye thamani ya shilingi 5,000/= ambaye hata ukienda kumuuza kwenye soko la mtaani huwezi kumuuza bei hiyo ndogo"  alilalamika mmoja kati ya wavuvi.


Licha ya wavuvi hao kuwafuata wamiliki wa viwanda vyote jijini Mwanza na kuwakumbusha kuhusu kikao hicho hakuna hata kiwanda kimoja kilithubutu kuhudhuria. Viwanda ambavyo havikutoa ushirikiano kwa wavuvi hao ni pamoja na TFP, VICK FISH, OMEGA FISH na MWANZA FISH.


Anguko hilo la bei linakuja wakati gharama za uvuvi ziko juu kwa mfano lita moja ya mafuta aina ya petroli inauzwa sh. 2500/= na kuna mitumbwi inatumia kuanzia lita 40 hadi 60, vilevile kuna gharama za chakula kwa kambi ya wavuvi, ukarabati wa mitumbwi, nyavu na mengineyo.


"Unyanyasaji uliokithiri wa viwanda vya kuchakata samaki dhidi ya wavuvi na wafanyabiashara wa samaki kanda ya ziwa unatia huruma ili kutibitisha kuwa kuna usanii kwa hawa mabwana tizama leo wameshindwa kuhudhuria mkutano huu wa maafikiano, kweli inakatisha tamaa lakini sisi tunaahidi kuwa tutapambana hadi kieleweke"


Tayari wavuvi kadhaa wanashikiliwa na jeshi la polisi Mwanza mara baada ya kuzuia mitumbwi kadhaa kuendelea na huduma kwa kudai kuwa ni wasaliti wa kauli ya umoja wa wavuvi sambamba na hilo tukio lingine linatajwa kutokea eneo la kiwanda cha Nile Peach, ambapo  wavuvi wanaofanya doria kubaini wasaliti walitoboa mtumbwi uliokuwa na barafu wa jamaa anayeitwa Kaswamila hata kuzama, ukitajwa kuwa ulikuwa ukienda ziwani kuchukuwa samaki kwaajili ya biashara na kiwanda hicho. 

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Sangara iliyokwisha safishwa yaani fillet kwa mlaji kwa kilo inauzwa dollar 8 ya kimarekani hapa dubai na ndiyo samaki ya rahisi kabisa, Lakini wateja wake sio wengi kwa wanunuzi wa samaki maji ya chumvi bei ni mbaya na wateja ni wengi.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.