ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 30, 2012

SIKU MOJA KABLA YA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA MKUU WA MKOA WA MWANZA ATEMBELEA MAONYESHO: KESHO WAZIRI MKUU MH. PINDA KUFUNGA.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza akiwa amebeba kombe la Ushindi wa Usafi kwa majiji lililotunukiwa kwa mkoa wake hivi karibuni kwa mwaka wa saba mfululizo, mkuu huyo akiwa ameambatana na Katibu wa CCM Mkoa bi. Joyce Masunga na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Polisaga amefanya ukaguzi leo kwenye mabanda ya maonyesho ya maadhimisho hayo yaliyopo ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo kesho  Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Pinda atafunga rasmi na kutoa zawadi kwa washindi. 

Injinia Ndikilo akipata maelezo ya viatu vilivyotengenezwa na ngozi asilia toka kwa moja ya wadau wa kutengeneza bidhaa zinazotumia ngozi.

Ni ramani za majengo matatu ya kisasa yatakayo jengwa ndani ya jiji la Mwanza ikiwa ni pamoja na Soko kuu, Jengo la kliniki kwa akinamama eneo la Utemini na Jengo la Idara ya Afya.

Wananchi wakipata maelezo  ya bidhaa za mikono.

Mdau akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lake.... "ulishawahi kula nsansa wewe?"

Nafaka zaweza kutumika kwa mapishi mengi .... "Ushawahi kula chapati za viazi wewe?"

Nafaka maonyeshoni.

Rozela inatumika kutengeneza wine (kama unavyoona pichani) wine iliyofull kiwango yenye manufaa kwa mwili kama kusafisha figo, kuongeza damu, kuburudisha akili na kuimarisha nguvu ya msisimko kwa mwili.

Mwananchi akijipatia yake moja kwaajili ya kujinafasi.

Afisa muuguzi bingwa wa magonjwa ya akili na kutoa dawa za usingizi toka Hospitali ya Wilaya ya Misungi, Bon Venture P. Michael akitoa maelezo kwa mwananchi.

Afisa nyuki mwandamizi toka wilaya ya Misungwi Thomas E. Mshana, akionyesha nta na mazalia ya nyuki yanayozalisha asali.

Benito Bernard Makombe kutoka Halmashauri ya jiji la Mwanza akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kushiriki zoezi la SENSA ya watu linalotaraji kufanyika mwezi agosti mwaka huu.

Eneo la tukio kwa chati na wana usalama.

Afisa uhusiano wa jiji la Mwanza Joseph Mlinzi akionyesha moja ya vikombe na vyeti ambavyo Halmashauri ya jiji imejinyakulia katika mashindano ya usafi na mazingira kwa mara ya saba mfululizo tangu kuanzishwa kwake, kesho Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo K. Pinda anatarajiwa kuhitimisha maonyesho hayo wananchi mnakaribishwa.
Kiingilio ni Bureeeeeee....

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.