Hatua hiyo inafuatia barua yake ya April 10 mwaka 2011 yenye kumb.Na DA/171/181/01N/97 Aliyowaandikia kikundi cha wachimbaji wadogo cha Ngasamo Native Mining Group na kuwakabidhi April 10 2012 akidai kuwa eneo hilo walilipo na kuendeleza shughuli za uchimbaji kumilikiwa na Kampuni ya Preucous Metals Refinery Company Ltd (PMRC) tangu mwaka 2005.
Wachimbaji hao wadogo wa wenye kikundi kilichosajiliwa kiitwacho Ngasamo Native Mining Group wanasema kuwa wamesikitishwa na hatua ya Kamishina msaidizi Salum S.Salum kuwatisha pamoja na kutumia wadhifa wake kuwaandikia barua ya kuwaondoa wachimbaji hao wadogo wakati akitambua kuwa eneo hilo wanalimiliki kihalali wakiwa na ramani yake na wana maeneo yao 15 yaliyosalia kati ya 40 wanayopaswa kugawiwa.
Wakizungumzia ujio wa Kampuni hiyo ya PMRC yenye leseni ya utafiti wa madini na si uchimbaji katika eneo lao wanasema kampuni hiyo iliingia katika eneo hilo kwa gia ya kuwasaidia vifaa vya kisasa vya uchimbaji kwa wachimbaji wadogo ili kuondokana na utumiaji wa nyezo duni kabla ya kuwageuka na kuanza shughuli za uchimbaji Madini na hatimaye kuchukuwa baadhi ya maeneo yao.
Suala jingine wachimbaji hao wadogo wanadai kwamba Kampuni hiyo ya PMRC yenye leseni ya kutafiti madini iliyopewa mikataba na kuongezewa mashimo sita kwa madai ya kuchukua mawe kuyapeleka Maabara ili kuyapima kugundua kama yana madini, haifanyi kama inavyopaswa bali huyapeleka inakojua kuyeyusha na kisha kufanyia biashara hali iliyopelekea kuna wakati wachimbaji kadhaa kupoteza dhahabu ya uzito wa zaidi ya kilogramu 3 kwa udanganyifu.
"Nasema haiwezekani kuondolewa katika eneo hili ispokuwa damu kumwagika tunamwomba rais Jakaya Mrisho Kikwete alishughulikie hili kwasababu ni mtu mwelewa na anajuwa wananchi wanapolalamika basikuna upindishwaji wa sheria na kanuni" mchimbaji mdogomdogo Shahbani Guya (Pichani).
Akizungumza kwa njia ya simu juu ya sakata hilo Kaimu Kamishina wa Madini wa Wizara ya Nishati na Madini Ally Samaje amekiri kuwepo kwa mgogoro huo katika eneo hilo la Igungumkilo na kusema kuwa ofisi yake iko kwenye mkakati kuhakikisha inakutana na wachimbaji wadogo na makampuni yaliyo na leseni ili kuondoa migogoro inajitokeza ikiwa ni pamoja na kukagua taratibu za barua iliyotoka ofisi ya madini kanda ya ziwa.
Wachimbaji hao wadogowadogo wameiomba serikali kupitia wizara ya madini kufuatilia suala hilo kwa kina ili wapate haki yao stahiki..
HATUA ZA MWISHO UPATIKANAJI WA DHAHABU
Mara baada ya mawe yenye dhahabu kupondwa vipande hupitishwa kwenye mashine maalum na kusagwa kisha kuwa kama vumbi ambalo huchotwa na kwenda kulowekwa kwaajili ya kuchujwa..
Hivi ndivyo vifaa vya kuchujia hatua ya kwanza, maji ya kawaida ndiyo yanahusishwa.
Uchujaji ukiendelea kwenye vifaa hivyo.
Hatua za mwisho kuisaka dhahabu...
Huku akiwa ameshikilia kipande cha dhahabu mdau mwananchi wa kawaida anaronga.... "Mimi ndiyo 'taita' wa mgodi huu"
Wachimbaji wadogo wakikusanya vifusi vya mawe yaliyo na dhahabu... sooon ntaku show moja kati ya mawe yenye dhahabu vile yanafanana kupitia video.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.