Mbunge wa viti maalum CCM mkoani Geita, mh Vick Kamata akisalimiana na mtoto ambaye ana ulemavu wa mguu kwa muda wa miaka 15 tangu sasa tangu alipozaliwa huyu ni mmoja kati ya waliokabidhiwa baiskeli ili kuwawezesha katika harakati za maisha hususani kwa kijana huyu kwenye kuisaka elimu.
Victoria Foundation kwa muda mrefu sasa imekuwa ikifanya jitihada kuyawezesha makundi mbalimbali katika jamii ambapo mpaka sasa wananchi wengi katika makundi hayo yameweza kukuza vipato vyao.
Kundi hili katika jamii limeweza kupata baiskeli ambazo ni imani kwamba zitafanikisha kurahisisha harakati mbalimbali za kujikwamua kiuchumi na kushiriki ujenzi wa taifa letu la Tanzania kwani walemavu wakiwezeshwa naaam wanaweza.
Baiskeli 30 zilizotolewa na Victoria Foundation kwa wananchi wenye ulemavu wilayani Nyakamwaga mkoa mpya wa Geita.
Ni baadhi ya walemavu wakiwa wamepanda baiskeli zao baada ya kukabidhiwa.
Ni kama fikra za ndugu zetu hawa zinasema "Sasa tutashiriki vyema kwenye shughuli mbalimbali za jamii yetu"
Ni wazi kuwa kijana huyu alikuwa akipata taabu sana kwenda shule hasa ukizingatia shule nyingi vijijini ziko mbali na makazi ya watu kwa mpango huu wa uwezeshaji kutoka Victoria Foundation utamsaidia kuepukana na adha hizo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.