ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 4, 2012

TEKNOLOJIA YA GOLI KWA SOKA INAKUJA

Rais wa shirikisho linalotawala mchezo wa kandanda duniani, Sepp Blatter ameonyesha matumaini ya kuweza kuwashawishi wataalamu wa sheria za mpira kupiga hatua na kuanza kutumia teknolojia wakati wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Teknolojia ya soka
Haya ni mabadiliko makubwa katika msimamo wa Blatter tangu mcheza kiungo wa England afunge bao dhidi ya Ujeremani lililokataliwa wakati wa fainali za Kombe la Dunia huko Afrika ya kusini.

Baraza la Kimataifa la mchezo wa mpira wa miguu litafanya tathmini ya matokeo ya hivi karibuni siku ya jumamosi tarehe 3 kabla ya kutuma majaribio yaliyofanywa kwa mashirika ili yafanyiwe uchunguzi kabla ya uwamuzi mwezi Julai.

Bw.Blatter ameiambia BBC kua, 'hatutaki kurudia yaliyotokea wakati wa Kombe la Dunia na wiki iliyopita nchini Italia.

Lakini Rais wa Shirika la mpira barani Ulaya Michel Platini bado hajakubaliana na utumiaji wa komputa kusimamisha mchezo ili kuchunguza uhakika wa tukio. Platini anapendelea kuongezea wasaidizi zaidi wa mwamuzi wa kati.

Majaribio yatafanywa kwenye mashindano ya vilabu kwenye mabara mbalimbali, mfumo wa wasaidizi wa mwamuzi watatumiwa kwenye mashindano ya Ulaya, yanayotazamiwa mwezi Juni.

Msimamo wa Platini ni kutaka mchezo ubaki mikononi mwa binadamu na sio mitambo. Msimamo wa Platini unaungwa mkono na Makamu wa Rais wa FIFA Prince Ali wa Jordan.

Mpango unaotazamiwa kuigwa ni ule wa Hawk-Eye, uliobuniwa na kampuni ya Sony- na kutumiwa katika mashindano ya Tennis na cricket.

Chanzo bbc swahili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.